July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Manyoni walia na uhaba wa maji

Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Dar es Salaam, Daniel Mtuka akisalimiana na wananchi wa Manyoni

Spread the love

WANANCHI wa jimbo la Manyoni Mashariki wamelalamikia ukosefu wa maji safi na salama kwa kipindi cha zaidi ya miaka 55 ya Uhuru. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Wakizungumza na Mwananahalisi Online wananchi hao walisema mji mzima wa Manyoni unahudumiwa na mtu mmoja ambaye anawapatia maji halmashauri na halmashauri inawasambazia wananchi ambapo maji hayo hayatoshi.

Walisema kutokana na wingi wa wakazi wa Mji wa Manyoni mahitaji ya maji ni takribani lita za ujazo laki saba lakini maji yanayopatikana ni laki mbili tu jambo ambalo linasababisha akina mama kutumia muda mwingi kutafuta maji na kukwamisha shughuli za maendeleo.

Mbali ya kulalamikia tatizo la maji wananchi hao walisema kuna tatizo kubwa la ukosefu wa huduma bora za Afya, elimu pamoja na kukithiri kwa migogoro ya ardhi.

Wananchi walitoa malalamiko yao mbele ya Danieli Mtuka wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Sokoni Stendi ya magari ya Vijiji kwa ajili ya kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya kuwania ubunge katika jimbo la Manyoni Mashariki kupitia CCM.

Wananchi hao walisema wilaya ya Manyoni ni kati ya Wilaya zenye vyanzo vingi vya mapato lakini bado imekuwa nyuma kimaendeleo.

Walisema sababu kubwa ya kutokuwa na maendeleo ni kutokana na kukosekana kwa kiongozi makini ambaye anaweza kusimamia hoja ambazo anatumwa na wananchi.

Kutokana na adha hiyo wananchi walisema kwa sasa umefika wakati wa kumpata mtu ambaye ni shupavu na na mwenye kuwasilisha hoja za wananchi bungeni.

Bila kutafuna maneno wananchi hao walisema mtu pekee ambaye anaweza kutatua kero za wananchi ni Daniel Mtuka kutokana na uzoefu alionao katika kushughulikia changamoto mbalimbali katika jamii.

Kwa upande wake Mtangaza nia Daniel Mtuka, ambaye kwa sasa ni Kamanda kiongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Dar es Salaam na Mlezi wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Manyoni, amesema umefika wakati sasa wa wananchi wa manyoni kuendelea matatizo.

Akuhutubia umati wa watu katika mkutano wa hadhara kwa lengo la kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Manyoni Mashariki, ambalo kwa sasa linaongozwa na John Chiligati, amesema wakazi wa Manyoni wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kutatuliwa kama atapatikana kiongozi shupavu.

Mtuka amesema jambo ambalo linamuumiza kichwa na anatamani kulitatua iwapo atapata ridhaa ya kuingia bungeni ni kero ya Maji, huduma ya afya pamoja na sekta ya elimu.

“Lazima kutafuta ufumbuzi wa kutatua kero ya maji, utatuzi wa migogoro ya ardhi,elimu pamoja na maswala yote ambayo yanawahusu vijana,akina mama na wazee.

“Ninajua katika jimbo la Manyoni kuna changamoto mbalimbali lakini kuna uwezekano mkubwa wa kuzitatua pale tu ninapoweza kupata ridhaa yenu wananchi ya kuingia pale bungeni.

“Mambo mengi yapo ndani ya uwezo wetu kwanza kabisa nimanshukuru huyu mtu ambaye anatusaidia kutupatia maji katika mji wa Manyoni lakini kuna sababu ya kumsaidi kwa kutafuta vyanzo vingine ya upatikanaji wa maji ni kweli anatusaidia lakini maji hayatoshi,” amesema .

error: Content is protected !!