May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Manula arejea kikosini

Spread the love

 

MLINDA mlango wa klabu ya Simba na timu ya Taifa ya Tanzania Aishi Manula emerejea kwenye kikosi cha klabu yake hii leo tare he 3 Machi 2021, mara baaada ya kutoka hospitalini alipokuwa akipata matibabu baada ya kuumia kwenye mchezo wa ligi Kuu dhidi ya Jkt Tanzania. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Manula ambaye aliruhusiwa kutoka hospitalini siku ya jana na kupatiwa mapumziko na madaktari wa timu hiyo ili kujiweka tayari kwa jailli ya safari ya kuelekea nchini Sudan kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa bara Afrika.

Taarifa ya kurejea kikosini kwa mlinda mlango huyo ilitolewa kupitia kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya klabu ya Simba ambayo ilionesha picha akiwa anaongea na kocha wa makipa wa klabu hiyo Milton Nienov.

Kipa wa Simba Aishi Manula (Kushoto) akiwa na kocha wa makipa Milton Nienov wakati akirejea kambini

Manual alipata Madhira halo mara bade ya kugongana na mchezaji wa Jkt Tanzania Daniel Lyanga wakati wakigombania mpira wa juu kwenye dakika ya 67 ya mchezo nakupelekea kupoteza fahamu na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.

kurejea kwa kipa huyo kumendelea kuwatia moyo mashabiki na viongozi wa klabu hiyo kutokana na kiwango bora alichokionesha kwenye michezo miwili dhidi ya As Vita na Al Ahly.

Kikosi cha Simba kinaondoka hii leo majira ya saa 10:45 jioni kupitia Ethiopia na kisha kesho kuingia nchini Sudan kwa jailli ya mchezo huh.

 

 

error: Content is protected !!