Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Manji kuongoza Mkutano Mkuu Yanga kesho
Michezo

Manji kuongoza Mkutano Mkuu Yanga kesho

Yusuf Manji
Spread the love

YUSUF Manji, anayejitambua kama Mwenyekiti wa Yanga, anatarajia kuongoa Mkutano Mkuu wa dharura wa klabu hiyo unaotarajia kufanyika kesho, ambao mpaka sasa haujafahamika utafanyika wapi wala ajenda za mkutano huo hazijajulikana. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Akiongea na moja ya kituo cha radio leo asubuhi Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo, Hussein Nyika amesema kuwa bado wanatafuta ukumbi ambao utaweza kutosha wanachama wote watakaohudhuria mkutano huo siku ya kesho ambao utakaoongozwa na Manji.

“Mkutano kesho upo palepale ila kwa sasa tunatafuta ukumbi utakaoweza kutosha kufanyikia mkutano huo, ambao utaongoza na Yusuph Manji ambao bado sisi tunamtambua kama Mwenyekiti wa Yanga na wanachama kufanya maamuzi,” amesema Nyika.

Hivi karibuni Manji aliandika barua ya kukubali ombi la wanachama kurudi katika nafasi yake kama Mwenyekiti ndani ya klabu hiyo kutokana na mapendekezo ya mkutano mkuu uliofanyika 10 Juni, 2018, na barua yake iliwasilishwa na Mwenyekiti wa baraza la Wadhamini, Kapteni George Mkuchika mbele ya wana habari.

Mkutano huo ambao unaenda kufanyika huku mchakato wa uchaguzi wa kujaza nafasi zilizoachwa wazi ukitarajia kufanyika 13 Januari, 2019, katika nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wanne wa kamati ya utendaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!