Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Yusuf Manji aachiwa huru, DPP afuta kesi
Habari MchanganyikoTangulizi

Yusuf Manji aachiwa huru, DPP afuta kesi

Yusuf Manji akiwasili mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia Huru Mfanyabiashara Yussuf Manji na wenzake kwenye uhujumu Uchumi baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka DPP kuwasilisha hati ya kutoendelea na Mashtaka mahakamani hapo, anaandika Faki Sosi.

Akiwasilisha hati hiyo Kishenyi Mutalemwa Wakili wa Serikali mbele ya Hakimu Mkazi, Huruma Shahidi ambapo ameeleza Mkuregenzi huyo hana nia ya kuendelea na Mashataka hayo. Manji alifikishwa kwenye mahakama hiyo majira ya saa 7 mchana akitokea mahabusu.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda (28), Mtunza stoo, Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43).

Awali Julai 5, mwaka huu, mahakama ililazimika kumfuata Manji kwenye wodi namba moja ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili alipokuwa amelazwa kutokana na ugonjwa wa moyo na kusomewa mashtaka ya uhujumu uchumi.

Aidha alidaiwa Juni 30, mwaka huu maeneo ya Chang’ombe A wilayani Temeke Dar es Salaam, washitakiwa wote kwa pamoja walikutwa na askari polisi wakiwa na mabalo 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vyenye thamani ya Sh. 192.5 milioni .

Pia washitakiwa wote walikutwa na askari polisi wakiwa na mabalo nane ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za JWTZ vyenye thamani ya Sh. 44 milioni .

Katika mashitaka ya tatu, inadaiwa Juni 30, mwaka huu maeneo ya Chang’ombe A, washitakiwa walikutwa wakiwa na mhuri wa JWTZ ambao uliandikwa “Mkuu wa Kikosi 121 Kikosi cha JWTZ” bila kuwa na uhalali kitendo kinachohatarisha usalama wa nchi.

Pia inadaiwa tarehe hiyohiyo maeneo ya Chang’ombe, washitakiwa walikutwa na mhuri uliokuwa umeandikwa “Kamanda Kikosi 834 KJ Makutupora Dodoma” bila kuwa na uhalali kitendo kinachohatarisha usalama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

error: Content is protected !!