Saturday , 22 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Manji apata pigo jingine akiwa mahabusu
Habari Mchanganyiko

Manji apata pigo jingine akiwa mahabusu

Spread the love

SERIKALI imekitaifisha kiwanda cha kuchakata ngozi cha Mwanza Tanneries kilichopo Ilemela mkoani Mwanza kwa kushindwa kuendelezwa na kuendeshwa kwa zaidi ya miaka mitano sasa, anaandika Moses Mseti.

Kiwanda hicho, kinachomilikiwa na mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji, ambaye anasota mahabusu jijini Dar es Salaam, kimekuwa na mgogoro wa muda mrefu kati yake na kampuni ya Caspian.

Kampuni ya Caspian inatajwa kumilikiwa na mfanyabiashara, Rostam Aziz ambaye awali ndiye alikuwa akikimiliki kabla ya kubadilisha umiliki wake kwenda katika kampuni za Manji miaka kadhaa iliyopita.

Manji anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na wenzake watatu, ikiwemo ya kukutwa na vitambaa vya sare ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), hata hivyo kufungwa kwa kiwanda hicho ni pigo jingine kwake kutokana na kuandamwa na kesi nyingi.

Akizungumza leo wakati wa kukitafisha na kukifunga rasmi kiwanda hicho baada ya muda wa siku 60 kutolewa kwa uongozi wake kuhakikikisha wanakiendelea, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, alidai kuwa serikali imepata hasara kubwa (hakuitaja) kwa kutoendelezwa.

Mongella amesema kuwa baada ya kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na umiliki halali wa kiwanda hicho wamebaini kuna utapeli ambao ulifanyika kutoka kwa mmiliki huyo pamoja na watumishi wa umma.

Amesema kiwanda hicho awali kilikuwa kikimilikiwa na kampuni ya Afrika Tanneries kisha kubadilishwa umiliki kwenda kwa kampuni ya Kasco ambayo na yenyewe inadaiwa imebadilisha umiliki wake kwa kampuni ya Quality Group ambayo inadaiwa imeshindwa kukiendeleza.

Mongella amesema kuwa upande wa Quality Group unadai kiwanda hicho ni mali yao na kampuni ya Kasco pia inadai wao ndio wamiliki halali wa kiwanda hicho kitendo ambacho kimesababisha mgogoro wa muda mrefu hivyo Serikali kuchukua hatua ya kukifunga mpaka pale mwaafaka utakapopatikana.

“Kuanzia sasa kiwanda hiki ni mali ya serikali na nyie (Quality group) hamna chenu humu na tumebaini serikali haijawahi kuuza kiwanda hiki kwenda kwa mtu yeyote na ieleweke kuanzia muda mmiliki ni serikali.

“Nilipokuja hapa tarehe 10 (Julai mwaka huu) niliagiza vyuma chakavu viondoke mara moja ili ndani ya miezi sita tuwe tumeanza uwekezaji hapa, lakini hakuna kilichofanyika, sasa hata hivi vifaa (vyuma chakavu mali ya Caspian) visitoke,” amesema Mongella.

Mongella amesema kuwa, serikali itakwenda kukaa na kuangalia hasara ni kiasi gani cha hasara imekipata kwa kipindi ambacho kiwanda hicho kilipokuwa hakifanyika kazi ili kuona namna ambayo wataweza kurudisha kodi yake.

Pia Mongella amesema kuwa serikali mkoani humo imeanza oparesheni ya kukagua viwanda vyote ambavyo vilibinafsishwa kinyemela bila kufuata utaratibu ikiwemo kiwanda cha kutengeneza kanga na vitenge cha Mwatex 2001 kilichopo Nyakato.

Mongella, amesema kuna nyumba sita zilizopo Bugando zilizokuwa zikimilikiwa na Tanneres na kwamba wamiliki wake walizipata kwa njia ya mkato huku akiwataka kujiandaa kisaikolojia kwani zitarudishwa kwenye mikono ya serikali.

Julai 10 mwaka huu, Msimamizi wa kiwanda hicho kutoka kampuni ya Quality Group, Chacha Mathew, alisema wao walilazimika kuzuia vyuma chakavu ikiwemo mitambo ya migodini kwa kuwa walikuwa wakiidai kampuni ya Caspian

Mathew leo wakati wa zoezi la kukitaifisha kiwanda hicho, amesema wao walikuwa ni wamiliki wa kiwanda hicho lakini walishindwa kukiendelea kwa muda mrefu jambo ambalo limesabaisha serikali kukitaifisha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washiriki mbio za NBC Dodoma Marathon kutumia treni ya SGR kwenda Dodoma

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

Habari MchanganyikoTangulizi

Padre anayetuhumiwa mauaji ya Asimwe, asimamishwa

Spread the loveKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji...

Habari Mchanganyiko

Upandaji miti uzingatie kuondoa umaskini kwa wananchi

Spread the loveKATIBU Tawala wa mkoa wa Morogoro Dk. Musa Ally Musa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

error: Content is protected !!