Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Manispaa yabanwa matumizi ya fedha za vijana
Habari za Siasa

Manispaa yabanwa matumizi ya fedha za vijana

Madiwani Manispaa ya Morogoro
Spread the love

MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wameitaka kuwekwa wazi kwa asilimia 5 ya mapato ya halmashauri hiyo ambayo yanapaswa kutolewa kama mikopo kwa vijana na wanawake, anaandika Christina Haule.

 Hatua hiyo inakuja kufuatia malalamiko ya wananchi wengi kuwa hawajui fedha hizo zimekuwa zikitumiwaje na halmashauri hiyo huku madiwani nao wakishindwa kuwa na majibu ya kuridhisha juu ya suala hilo.

Doroth Mwamsiku, diwani wa viti maalum akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo amesema, taarifa za mikopo hiyo kwa wanawake na vijana zinapaswa kuwa wazi ili wananchi waweze kunufaika na fedha hizo.

“Taarifa hizo zinatakiwa kuwa wazi kwa kila kata ili ijulikane ni vikundi gani vinapata fedha hizo sambamba na kuwepo kwa taarifa za mrejesho wa mikopo hiyo.

“Tunapofika kwenye mikutano na wananchi tunakumbana na maswali mengi, likifika hilo la mikopo ya makundi hayo ndipo sisi madiwani tunapokosa majibu ya kutosha,” amesema.

Akijibu hoja hiyo Pascal Kihanga, Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo amewataka madiwani kujenga mahusiano ya karibu na viongozi wa kata ili waweze kupata taarifa hizo.

“Taarifa za matumizi ya fedha hizo zipo, kinachotakiwa ni nyie kuwa na mahusiano mazuri na watendaji wa kata ambayo yatawafanya mpate majibu sahihi mnapofika kwenye mikutano na wananchi,” amesema Kihanga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!