Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Manispaa Temeke matatani, Magufuli aagiza uchunguzi
Habari za SiasaTangulizi

Manispaa Temeke matatani, Magufuli aagiza uchunguzi

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, John Magufuli amenusa ufisadi wa Sh.19 bilioni, Manispaa ya Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam na kuagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuifanyia uchunguzi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Ijumaa tarehe 26 Februari 2021, wakati anaweka jiwe la msingi ujenzi wa Kiwanda cha Ushonaji katika Bohari Kuu ya Jeshi la Polisi, Kurasini, Dar es Salaam, ikiwa ni siku ya tatu nay a mwisho wa ziara mkoani humo.

Kiongozi huyo wa nchi, amebaini ufisadi huo katika Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP), baada ya Mbunge wa Temeke (CCM), Dorothy Kilave, kumuomba aisaidie manispaa hiyo kumalizia deni la Sh.12.1 bilioni inayodaiwa na Benki ya CRDB.

Manispaa ya Temeke, ilikuwa inadaiwa Sh.19 bilioni, ilizokopa katika benki hiyo, kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi ambao maeneo yao yalichukuliwa na manispaa hiyo kwa ajili ya kujenga zahanati na barabara kupitia mradi wa DMDP.

Rais Magufuli, ameagiza Takukuru ifanye uchunguzi kubaini fedha hizo zilitumikaje kwani wakati wanajadiliana kuhusu mkopo huo unaowagharimu Sh.4.8 bilioni kila mwaka, serikali haikuhusika.

“Mbunge najua ulikuwa haupo, lakini lazima nikutandike sababu wamekutuma kuzungumza hapa. Hakuna hela itakayotolewa sana sana nitatuma wakaguzi wa kuchunguza. Makamanda wa Takukuru mnisaidie kufanya uchunguzi,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema, “tujue nani alikwenda kuzungumza na CRDB, maeneo yalikuwa ya nani, fedha zilizolipwa kweli zilikuwa zinastahili? Kama bilioni 12, je yale majengo yana thamani ya bilioni 12. Nani alikwenda kufanya mazungumzo na CRDB?”

“Mmeshindwa kulipa mnataka serikali ilipe deni, kwa hiyo tuna manispaa ngapi, halmahuri ngapi, zikafanye mamikopo yao ya wizi serikali ije kulipa? Hilo mlisahau, mtalibeba wenyewe,” amesema Rais Magufuli.

Awali, Mbunge huyo aliyeanza kuliongoza jimbo hilo mwaka 2020 baada ya uchaguzi kumalizika alisema, manispaa hiyo imeelewa na deni hilo, kwani hutakiwa kulipa Sh.4.8 bilioni kila mwaka, fedha ambazo haiwezi kumudu kuzilipa na kusababisha kushindwa kutoa huduma kwa wananchi.

 

Aidha Kilave, alimuomba Rais Magufuli kuziangalia kata zisizoguswa na mradi huo, ili zinufaike nao.

“Katika mradi wa DMDP, kuna kata zimeguswa, katika DMDP phase 2 (awamu ya pili) tuombe kata ambazo hazijaguswa tuweze kugusa,”amesema Kilave.

“Unapokutana na mfalme, naomba niseme mambo machache na naomba uyapoke, Manispaa ya Temeke tulikopa fedha CRDB kulipa mafao ya wale tunakwenda kubomoa sehemu zao kujenga maendeleo DMDP.”

“Tumepeta bilioni 19 za kulipa watu kujenga zahanati na barabara, deni lile limekuwa kubwa, tumeweza kulipa kwa awamu, kila mwaka bilioni 4.8. Kutokana na mahesabu ya ndani, tunalipa awamu nne, Bilioni 1.2 kila robo ya mwaka. Deni limekuwa changamoto naomba ulipokee,” aliomba Kilave.

Mbunge huyo amesema, kama Serikali italipokea deni hilo, fedha zilizopangwa kutumika kulilipa zitaelekezwa katika kufanya miradi ya maendeleo ndani ya manispaa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!