WAFANYABIASHARA wametakiwa kuzingatia masharti ya leseni za biashara na vileo ili kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya serikali, anaandika Pendo Omary.
Akizungumza na MwanaHALISI Online, Peter Ngoti, Ofisa Biashara Halmashauri ya Kinondoni amesema, masharti hayo yanayosimamiwa na Sheria namba 25 ya Leseni na Biashara ya Mwaka 1972, inamtaka mfanyabiashara kukata leseni ya biashara, kutokuweka leseni mahali pasipoonekana na kutokumzia afisa wa serikali kufanya ukaguzi.
“Masharti mengine ni; kutotoa taarifa za udanganyifu wakati wa kukata lessen, kutotumia leseni moja katika biashara mbili tofauti au kutumia leseni mbili katika biasahara moja na kuonesha leseni ya biashara mara mfanyabiashara anapopaswa kufanya hivyo,” amesema Ngoti.
Ngoti amesema kwa mwaka 2014/2015 ukataji leseni umeongezeka ambapo leseni za biasahara 22,070 zilikatwa huku leseni za vileo 4,289 zikikatwa ukilinganisha na mwaka 2013/2014 ambapo leseni za biasahara 17,277 zilikatwa huku leseni za vileo 4,289 zikikatawa.
More Stories
NMB yamwaga vitanda, magodoro Kagera
NBC wasisitiza kukuza michezo, sanaa na utamaduni
TPA yatangaza vipaumbele muhimu 5