Friday , 9 June 2023
Home Kitengo Maisha Afya Manesi 7 mbaroni tuhuma za kuwauzia dawa wagonjwa usiku wa manane
Afya

Manesi 7 mbaroni tuhuma za kuwauzia dawa wagonjwa usiku wa manane

Spread the love

 

JUMLA ya wauguzi/manesi saba wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama wamefikishwa polisi baada ya kudaiwa kuwauzia dawa wagonjwa usiku wa manane. Anaripoti Paul Kayanda, Shinyanga … (endelea).

Wauguzi hao wanadaiwa kudakwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakiwa na dawa za aina mbalimbali kwenye pochi zao za mkononi (handbag).

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Anderson Msumba amesema wauguzi hao walikutwa na dawa mbalimbali ikiwamo drip za maji, dawa za kuongeza na nyingine.

Amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakipata malalamiko kutoka kwa wagonjwa kwamba wanauziwa dawa na manesi hao kutoka kwenye mikoba yao.

“Tulikuwa tunafanyia kazi hizi tuhuma hizo ambapo wenzetu wa Takukuru walifanya ukaguzi wa kushtukiza tarehe 24 Februari 2023 katika baadhi ya wodi na kawakuta wawakilishi wakiwa na dawa kwenye handbag zao.

“Waliwachukua na wakawahoji, baada ya kujiridhisha, nilienda hospitali nikakaa na uongozi na wafanyakazi na kuzungumza nao kwa kina.

“Nikawaagiza kutumia geti ambalo kila asubuhi msimamizi wa wodi alete taarifa ya utendaji kuhusu wodi husika kwamba mgonjwa kaandikiwa dawa gani na amezipata au lah ili haya masuala ya kuuziwa wodini yaishe,” amesema.

Amesema dawa hizo zinaweza kuleta madhara kwa wagonjwa kwani kwanza hawajui zimetoka wapi, pili haifahamiki ubora wake hivyo ni hatarishi kwa mgonjwa lakini pia hujuma hiyo inaikosema manispaa mapato.

“Ndio maana tukawapeleka polisi ili waendelee kuchunguzwa na kusearch-iwa, walichukuliwa maelezo na waliokidhi vigezo walidhaminiwa ila polisi bado wanaendelea na uchunguzi.

“Uchunguzi ukikamilika tutapata mrejesho na hatua zitachukuliwa ikiwamo kupelekwa mahakama,” amesema.

1 Comment

  • Ongela pccb kahama! Ukifuatilia juhudi za kushika dawa inaonyesha wazi mnafanyakazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

TEMDO yaanza kuzalisha vifaa tiba, bilioni tatu kutumika

Spread the loveKATIKA kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa vifaa tiba nchini,...

Afya

Ummy Mwalimu:Umeme wa uhakika tija kwa uboreshaji huduma za afya

Spread the loveWAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na...

Afya

Madaktari bingwa 10 waliokuwa India warudi na shuhuda nzito kuhusu utalii tiba

Spread the loveMADAKTARI bingwa wa upasuaji wa ubongo wameendelea kuongezeka katika Taasisi...

Afya

Kipindupindu chabisha hodi Dar, wagonjwa 10 waripotiwa

Spread the love  Ugonjwa wa Kipindupindu umeibuka jijini Dar es salaam ambapo...

error: Content is protected !!