Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Maneno ya mwisho ya Magufuli kwa Rais Samia
Habari

Maneno ya mwisho ya Magufuli kwa Rais Samia

Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Dkt John Magufuli
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani, amesema siku chache kabla ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Hayati John Pombe Magufuli kufariki dunia, alimpa ujumbe wa kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa 202, ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Kiongozi huyo mpya wa Tanzania, amesema hayo leo Jumatatu tarehe 22 Machi 2021, wakati akihutubia maelfu ya waombolezaji kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma, ambapo mwili wa Dk. Magufuli, umeagwa kitaifa.

“Nilipata fursa ya kuongea naye siku chache kabla ya kifo chake, pale nilipo mtaarifu nakwenda kwenye ziara Tanga, naye aliniambia Samia usiwe na wasiwasi naendelea vizuri, nenda kafuatilie ilani ya CCM, kama tulivyo waahidi wananchi tutaitekeleza,” amesema Rais Samia.

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania

Kifo cha Rais Magufuli kilitokea tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu ya matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo.

Kongozi huyo wa kwanza kuwek historia ya kuwa rais wa kwanza mwanamke Tanzania, alitangaza kifo cha Hayati Rais Magufuli, akiwa ziarani mkoani Tanga.

Ambapo alilazimika kusitisha ziara yake hiyo iliyopangwa kufanyika kwa siku tano mkoani Tanga, kuanzia tarehe 15 hadi 19 Machi 2021.

Akizungumzia wosia huo wa Hayati Rais Magufuli, Rais Samia amesema hakujua kama maneno hayo yalikuwa ya mwisho kutoka kinywani mwa kiongozi huyo.

“Wape salamu zangu Watanzania, waambie nawapenda sana. Na hayo ndio yalikuwa maneno yake na mimi ya mwisho, sikujua kwamba maneno yale yalikuwa ya kuniaga na kuwaaga Watanzania, sikujua kwamba sitapokea simu zake tena ZA asubuhi wewe bado umelala, sitasoma mwandiko wake tena,” amesema Rais Samia.

Mwili wa Hayati Rais Magufuli aliyeongoza Tanzania kwa miaka sita mfululizo (2015-2021), utazikwa Ijumaa tarehe 26 Machi 2021, kijijini kwao Chato mkoani Geita.

Dk. Magufuli, ameacha mjane, Janeth na watoto saba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariHabari Mchanganyiko

CRB yashtukia makandarasi wanaofanya ubia wa ujanja ujanja, yasema watakaobainika kuchukuliwa hatua kali

Spread the love  BODI ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imeonya makandarasi wanaofanya...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Habari

Mnyika aacha ujumbe msibani kwa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Taifa, John...

HabariHabari Mchanganyiko

Mwili wa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine wawasili, kuzikwa Mbeya

Spread the loveMWILI wa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, aliyefia...

error: Content is protected !!