Saturday , 30 September 2023
Home Kitengo Michezo Mandonga nje miezi 6, kufanyiwa vipimo Muhimbili
Michezo

Mandonga nje miezi 6, kufanyiwa vipimo Muhimbili

Spread the love

BONDIA wa ngumi za kulipwa, Karim Mandonga anatarajiwa kufanyiwa kipimo cha kichwa baada ya kupata jeraha kutokana na kipigo alichokipokea tarehe 29 Julai 2023 jijini Mwanza.

Mandonga  alipigwa kwa TKO na Moses Golola wa Uganda katika pambano la raundi nane lisilo la ubingwa la uzito wa juu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kutoka na kipigo hicho, Mandonda (42) aliumia kichwa na kuifanya Kamisheni ya Ngumi ya Kulipwa Tanzania (TPBRC, kutangaza kumsaidia kupata vipimo kisha matibabu katika Hospitali ya Muhimbili.

Katibu wa TPBRC, George Lukindo amesema pamoja na kupelekwa kupata vipimo, Mandonga hataruhusiwa kucheza pambano lolote kwa kipindi cha miezi sita.

Amesema shirikisho litasimamia uchunguzi wa afya ya bondia huyo na kumsimamia kwa karibu kwa mujibu wa kanuni ya mchezo wa masumbwi baada ya bondia kupigwa kwa TKO au KO.

Kocha wa Mandonga, Said Kisopu amethibisha kupokea barua ya TPBRC ya bondia wake kutakiwa kwenda kufanya vipimo vya afya chini ya shirikisho.

Kisopu amesema pamoja na shirikisho kusimamia vipimo vya bondia wake, uongozi utahakikisha Mandonga anapata matibabu ya kina na kurudi ulingoni baada ya miezi sita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Meridianbet yaibukia Tandika, yafungua duka jipya

Spread the love BAADA ya kupita maeneo mbalimbali hatimae kampuni yaMeridianbet imeibukia...

BiasharaMichezo

Ukiwa na Meridianbet ni rahisi kuwa milionea

Spread the love  CARABAO Cup raundi ya 3 Uingereza inaendelea na mechi...

Michezo

Jezi ya Samatta iliyoifunga Liverpool kuuzwa Genk

Spread the love  KLABU ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji imeamua kuanza...

BiasharaMichezo

Hii ndio historia ya El-Clasico, derby bora zaidi duniani

Spread the love  KILA nchi ina vilabu viwili hasimu na pinzani nje...

error: Content is protected !!