October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Manara kuifikisha Simba Mahakamani

Haji Manara, Msemaji wa klabu ya Yanga

Spread the love

 

ALIYEKUWA Afisa Habari wa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, klabu ya Simba, Haji Manara amepanga kuifikisha klabu hiyo mahakamani kwa kuwadai fidia mara baada ya kumtumikisha bila Mkataba kwa kipindi cha miaka sita. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Manara ambaye kwa sasa ni msemaji wa klabu ya Yanga, aliachana na waajiri wake wa zamani Julai, 2021 mara baada ya kutokea sintofahamu ndani ya klabu hiyo.

Akizungumza jana kwenye kipindi cha Lavidavi kinachorushwa hewani na kituo cha radio cha Wasafi na kufunguka kuwa, amepanga kwenda mahakamani ili alipwe fedha zake kutokana na kumfanyisha kazi kinyume na utaratibu.

“Wiki ijayo naenda Mahakamani, nawadai Simba fidia nyingi na wanapaswa wanilipe, wamenitumikisha bila mkataba, hawakunikatia NSSF, watanilipa fedha nyingi,” alisema Manara.

Mohammed Dewji ‘MO’

Msemaji huyo alingezea kuwa jambo hilo alitakiwa afanya hivi ndani ya wiki hii, lakini alimua aachane nalo kutokana wadai wake, klabu ya Simba kuwa na michezo ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hivi karibuni.

“Nilitakiwa niende wiki hii lakini niliombwa na kiongozi mmoja wa serikali niache, kwa kuwa wana mechi za Ligi ya Mabingwa, nimeacha wamalize mechi zao halafu nitakwenda, kwa sababu nikifanya sasa hivi itaonekana kama vurugu,” aliongezea Haji.

Simba tarehe 17 Oktoba 2021, itashuka dimbani nchini Botswana kutupa karata yake ya kwanza, kwenye hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy.

error: Content is protected !!