September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Manara hamisha tambo za Simba kwa Yanga

Spread the love

 

MSEMAJI wa Mabingwa wa Kihistoria Tanzania, Yanga ya Dar es Salaam, Haji Manara amesema, wanakwenda kuibuka na ushindi wa kutosha katika mchezo wao dhidi Rivers United ya Nigeria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Yanga itashuka dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kuanzia saa 11 jioni ya Jumapili hii ya tarehe 12 Septemba 2021, kuumana na Rivers United, kwenye mchezo wa awali wa Klabu Bingwa Afrika.

Leo Jumanne, tarehe 7 Septemba 2021, Manara akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Yanga, Dar es Salaam alipokaribishwa rasmi amesema, wanakwenda kuibuka na ushindi ili kurahishia mchezo wa marudiano utakaopigwa Nigeria, wiki mbili zijazo.

 

“Tunakwenda kushinda kwa matokeo ambayo mechi inakwenda kumalizikia nyumbani,” amesema Manara ambaye amejiunga na Yanga akitokea Simba.

Amesema, kesho Jumatano atazungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo akidokeza “tutakuja na slogan nzito ambayo itaamusha kutoka kwa wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki wote.”

error: Content is protected !!