Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Michezo Manara awaomba radhi Yanga ‘niliteleza’
Michezo

Manara awaomba radhi Yanga ‘niliteleza’

Haji Manara, Msemaji wa klabu ya Yanga
Spread the love

 

HAJI Sunday Manara, Msemaji wa Mabingwa wa Kihistoria nchini Tanzania, Yanga ya jijini Dar es Salaam amewaomba radhi wanachama na mashabiki wa timu hiyo kwani “kuna mahali niliteleza.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Manara amewaomba radhi leo Jumanne, tarehe 7 Septemba 2021, alipokaribishwa rasmi makao makuu ya Yanga, Jangwani jijini Dar es Salaam baada ya kujiunga nao hivi karibuni akitokea kwa watani zao Simba.

Amepokewa na wazee wa timu hiyo ambapo kabla ya kuingia ndani ya ofisi hizo zilizopo mtaa wa Jangwani na Twiga, Manara alinawishwa maji ikiwa ni ishara ya kusafishwa kutoka huko alikokuwa kuingia Yanga.

“Nimerudi kwenye klabu iliyonilea na ya maisha yangu. Wazazi wangu licha ya kucheza na kufanya kazi hapa lakini ndiyo ilinilea.”

“Wazee wangu kama kuna mahali lazima niliteleza kiungwana kabisa naombeni msahama wa dhati kabisa. Lazima niliteleza tu na mchukulie kuteleza kwangu ndiyo ilikuwa fursa ya kuja kufanya kazi kwa mabingwa wa kihistoria ‘home of championi,” amesema Manara

Manara amejiunga na Yanga akitokea kwa watani zao Simba nayo ya jijini humo alikoitumikia kama shabiki na msemaji kwa kipindi kirefu na kwa mafanikio makubwa.

Alianza kuzungumza kwa kuwashukuru mashabiki, wanachama na viongozi wa timu hiyo jinsi walivyompokea katika maeneo mbalimbali ikiwemo mitandaoni.

“Katika siku ngumu ni leo, unapokewa na watu ambao wewe unapaswa wakupokea, kwa mila na desturi wazee wanapokewa na vijana ila leo nimepokelewa na wazee wangu.”

“Deni hili pia ninalo kwa wanachama na mashabiki wa Yanga nchi nzima, kwa jinsi nilivyofanya kazi kule na kwa mapokezi siku ya kilele cha wiki ya mwananchi na mitandaoni, nina deni kubwa na halina budi kulipwa kwa kufanya kazi kwa kujitoa sana, kufanya kazi weledi mkubwa,” amesema

“Katika siku ngumu ni leo, unapokewa na watu ambao wewe unapaswa wakupokee, kwa mila na desturi wazee wanapokewa na vijana ila leo nimepokelewa na wazee wangu.”

Manara amesema “deni hili pia ninalo kwa wanachama na mashabiki wa Yanga nchi nzima, kwa jinsi nilivyofanya kazi kule, kwa mapokezi siku ya kilele ya wiki ya mwananchi na mitandaoni, nina deni kubwa na halina budi kulipwa kwa kufanya kazi kwa kujitoa sana, kufanya kazi wa weledi.”

Msemaji huyo mwenye maneno mengi amesema, Yanga ni nyumbani kwani amezaliwa mane ohayo ikiwemo kucheza ndani yta jingo hilo, kwenye vyumba vya wachezaji kwa maana hiyo “nimerudi kwelikweli nyumbani sehemu iliyonikuza.”

Awali, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha amemkaribisha Manara Yanga akisema Imani yake watafanya kazi pamoja kwa mafanikio makubwa “karibu sana nyumbani.”

Senzo na Manara waliwahi kufanya kazi pamoja wakiwa Simba na kila mmoja akiwa kwenye nafasi hizo hizo ambazo sasa wanazitumikia wakiwa Yanga.

1 Comment

  • Hongera sana kwa kuomba msamaha Manara.

    Tabia ya kuomba msamaha ni muhimu sana kwenye maisha ya mafanikio makubwa yenye furaha.

    Kuomba msamaha huongeza thamani kwa mwombaji msamaha. Hii ni tofauti na wengi wanavyofikiria.

    Ukikosewa omba msamaha. Ukimkosea mtu omba msamaha. Unatakiwa ujifunze kuomba msamaha kutoka moyoni mwako.

    Usiombe msamaha kwa sababu tu ndiyo utaratibu wako.

    Tabia hii utakuweka huru na utaweza kufanya kazi zako kwa amani.

    Rafiki yako,

    Aliko Musa.

    Real estate investment consultant

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!