Saturday , 13 April 2024
Home Kitengo Michezo Manara ang’aka Simba kupigwa sita Uturuki
Michezo

Manara ang’aka Simba kupigwa sita Uturuki

Spread the love

MSEMAJI wa Simba, Haji Manara amewashutumu vikali chombo cha Habari cha Clouds FM, kwa kutangaza taarifa za uongo kuhusu klabu ya Simba kucheza mchezo wa kirafiki na kufungwa mabao 6-0 nchini Uturuki ambayo timu hiyo imeweka kambi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Manara ameyasema hayo kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo alikitaka chombo hicho cha habari kuthibitisha au kukanusha taarifa hiyo waliyoitoa yenye nia hovu ya kuidhalilisha klabu ya Simba.

Msemaji huyo wa Simba ameandika katika ukurasa wake maneno haya: “Ngugu zangu wa Clouds with do respect mnachotufanyia c haki na mnatokosea sana ten asana!! Leo mmetangaza kwenye radio yenu Simba imecheza mechi uturuki na kufungwa 6-0.. tunaomba mthibitishe au mkanushe … vinginevyo mtakuwa na nia ovu ya kutudhalilisha na kwa hili hatutawaelewa na hatutakubali!! Mm wajibu wangu pia ni kulinda image ya club yangu na sipo tayari kuona chombo chochote kikitangaza taarifa ya uzushi na uongo dhidi ya Simba kwa kisingizio chochote kile.. kwa hili nategemea mtachukua hatua stahiki haraka iwezekanavyo .. vinginevyo thibitisheni.”

Simba ambayo kwa sasa imeweka kambi nchini Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Usiku wa Ulaya kinawak tena leo

Spread the love  LIGI ya mabingwa barani ulaya itaendelea tena leo ambapo...

Michezo

Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ni Usiku wa Kisasi

Spread the love  LEO utarejea ule usiku pendwa kabisa kwa mashabiki wa...

BurudikaMichezo

Kizz Daniel aunguruma na EP mpya ‘Thankz alot’

Spread the loveMKALI wa muziki nchini Nigeria, Kizz Daniel ametoa EP yake...

MichezoTangulizi

Samia aipa tano Yanga

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ameipongeza Klabu ya Yanga licha ya...

error: Content is protected !!