Thursday , 13 June 2024
Home Kitengo Michezo Manara afunguka nafasi yake kuchukuliwa Simba
Michezo

Manara afunguka nafasi yake kuchukuliwa Simba

Spread the love

MSEMAJI wa Simba, Haji Manara ametolea ufafanuzi swala la nafasi yake kama mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano ndani ya klabu hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … endelea.

Hayo yameibuka baada ya kuwepo kwa taarifa ya kutangazwa kwa nafasi hiyo kuchukuliwa na Gift Macha bila ya kufafanuliwa hatna ya Manala.

Manara ameeleza kuwa kwa sasa yeye ndio msemaji wa Simba na wala uongozi haujampa taarifa yoyote juu ya nafasi hiyo na hakuna matatizo kwenye uongozi.

Amesema pamoja na kuwa katika nfasi hiyo hadi sasa, lakini hawezi kukaa katika kiti hicho milelele itafika wakati atampa kijiti mtu mwengine na kuongezea kuwa taarifa hizo yeye anaziona kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa watu wengine.

“Kiti hiki nilichokalia cha usemaji wa Simba sitakaa nacho milele na wala hakuna mtu yoyote atakayekalia nafasi yoyote ya uongozi ndani ya klabu milele kwa kufa au kuondoka ila ipo siku lazima ukiachie na huo nduo uhalisia, mimi nadhani kwa sasa ibaki kwamba msemaji wa Simba ni Haji Manara na kama itatokea vinginevyo ndio asili ya kazi na hakuna tatizo lolote kwenye uongozi na mimi sijaambiwa kama kuna tatizo lolote,” alisema Manara.

Aidha Manala aliongezea kuwa klabu ya Simba ni kubwa kuliko mtu yoyote na wala timu hiyo sio mali ya mtu mmoja na hata siku ikitokea wao waliopo sasa wameondoka, basi hao wanaokuja wapewe ushilikiano na wanachama wote wa Simba.

Katika hatua nyingine klabu hiyo imetangaza kuwa siku ya Jumapili 25 Agosti, 2019 watacheza mchezo wa marudiano wa michuano ya klabu bingwa Afrika katika hatua ya awali kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Saalam dhidi ya UD Songo kutoka Msumbiji ambaoo mchezo wa kwanza uliisha kwa sare ya bila kufungana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo Tanzania ipo dimbani beti na Meridianbet

Spread the love  Mechi nyingi za kufuzu Kombe la Dunia kwa Afrika...

Michezo

Meridianbet inakwambia beti mechi spesho za EURO sasa

Spread the love Wakali wa ubashiri Tanzania Meridianbet wamekuja na Spesho ODDS...

Michezo

Jumamosi ni zamu yako kufurahia mkwanja na Meridianbet

Spread the loveWikendi ndiyo hii imefika jaman na wewe kama mteja wa...

Michezo

ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1,000 yapo hapa

Spread the love Mechi za mataifa za kufuzu kombe la Dunia 2026...

error: Content is protected !!