Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Manabii wa uongo wachongewa bungeni, Naibu Spika aingilia kati
Habari za SiasaTangulizi

Manabii wa uongo wachongewa bungeni, Naibu Spika aingilia kati

Mbunge wa Konde, Zanzibar (ACT-Wazalendo), Khatibu Said Haji
Spread the love

 

MBUNGE wa Konde, Zanzibar (ACT-Wazalendo), Khatibu Said Haji, amehoji Serikali inachukua hatua gani, kuwadhibiti manabii wa uongo na waganga wapiga ramli chonganishi ili wasiwatapeli wananchi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Haji amehoji hayo leo Jumatatu, tarehe 17 Mei 2021, katika kipindi cha maswali na majibu, bungeni jijini Dodoma.

“Je, serikali inachukua hatua gani, kukabiliana na waganga wapiga ramli chonganishi na manabii wa uongo, wanaodanganya na kuwatapeli wananchi kila siku,” amehoji Haji.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Hamza Chilo, amesema Serikali inachukua hatua mbalimbali kukabiliana na changamoto hiyo, ikiwemo kuwakamata wanaotuhumiwa.

“Operesheni na misako ya mara kwa mara imekuwa ikifanyika katika kuwakamata waganga wapiga ramli chonganishi na manabii wa uongo, wanaodanganya na kuwatapeli wananchi na kuwaletea hasara kubwa na mfarakano katika jamii kwa kuwachukulia hatua kwa mujibu wa Sheria,” amesema Chilo.

Chilo amesema “Katika kipindi cha mwaka 2020 wapiga ramli chonganishi 57 walikamatwa na kufikishwa mahakamani na kesi zao zipo katika hatua mbalimbali.”

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Hamza Chilo

Baada ya majibu hayo, Mbunge wa Mtambwe (ACT-Wazalendo), Khalifa Mohamed Issa, ameishauri Serikali ikae na manabii wanaodai kuwa na uwezo wa kufufua watu, ili wafufue maiti.

“Serikali haioni sasa wakati umefika kwa wale manabii ambao wanadai wanao uwezo wa kufufua waliokufa ili kukaa nao kwa karibu ili kuweza kuwafufua wapendwa wetu,” amehoji Issa.

Akijibu kuhusu ushauri huo, Chilo amesema, Serikali itakaa na wahusika kwa ajili ya kuwaelimisha ili waachane na vitendo hivyo kwa kuwa vinaleta migogoro kwa jamii.

Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika

“Imani ya kibinadamu ina amini na ndivyo ilivyo kwamba, mwenye uwezo wa kuondosha na kurejesha uhai wa mtu au kufanya mtu akafa na akafufuka ni Mungu peke,” amesema Chilo na kuongeza:

“Kama kutakuwa na watu wa namna hii kama alivyoshauri mbunge, tuko tayari kukaa nao tuwaleweshe, tuwaelimishe ili tuondoe migogoro katika jamii.”

Kufuatia mjadala huo, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson aliwashauri wabunge waache kujadili masuala ya imani, kwa kuwa Watanzania wana uhuru wa kuabudu.

“Waheshimiwa wabunge tujitahidi kujizuia hasa kujadili mambo ya imani, yanaleta changamoto kwa sababu wako watu wana amini akiumwa akiombewa anapona na nchi hii ina uhuru wa kuabudu. Nchi haina dini lakini watu wanaouhuru wa kuabudu,” amesema Dk. Tulia .

Naibu Spika huyo wa Bunge amesema, ni ngumu Serikali kuingilia kati suala hilo, kwani haitaweza kuwatambua manabii wa ukweli na uongo.

“Nchi hii haina dini lakini watu wanao uhuru wa kuamini, hata vitabu vya dini vinasema wako manabii wa ukweli na uongo, Serikali sina hakika kama mnao uwezo wa kuwatambua wapi wa uongo, wapi wa ukweli,” amesema Dk. Tulia na kuongeza:

“Wapiga ramli sawa kujadili sababu ni suala lingine, lakini mambo ya imani yataleta changamoto, humu ndani tukitaka kuliweka wale wananchi ambao wanaimani yao huko, pengine wapo ndugu zao walifufuliwa. Mimi sijui, hakuna ndugu yangu aliyefufuliwa labda kwa wengine wapo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

error: Content is protected !!