May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Man U yaipiga Roma 6-2, Arsenal yapigwa

Edson Cavan akishangilia moja ya bao alilofunga katika mchezo huo

Spread the love

 

MANCHESTER United ya Uingereza, imetoa kipigo cha ‘mbwa koko’ cha 6-2 kwa As Roma ya Italia, katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Ueropa, Barani Ulaya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ushindi huo wa kishindo, imeupata katika mchezo uliochezwa jana usiku Alhamisi, tarehe 29 Aprili 2021, Uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford.

Magoli ya Man U yamefungwa na Bruno Fernandes, Paul Pogba,Mason Greenwood na Edinson Cavani aliyetupia magoli mawili huku yale ya Roma yakifungwa na Lorenzo Pellegrini na Edin Dzeko.

Wakati Man U ikitoa kipigo hicho, washindani wao Arsenal ya Uingereza, yenyewe ikiwa ugenini nchini Hispania kucheza na Villarreal, ilipokea kipigo cha 2-1.

Wachezaji wa Villarreal wakishangilia baada ya kufunga bao katika mchezo wao dhidi ya Arsenal

Magoli ya Villarreal yalifungwa na Manuel Trigueros na Raul Albiol huku lile la kufutia machozi la Arsenal likifungwa na Nicolas Pepe.

Pia, mchezo huo, ulishuhudia kadi mbili nyekundi kwa Etiene Capoue wa Villarreal dakika ya 80, baada ya kupewa kadi ya pili ya njano sawa na Daniel Celallos wa Arsenal dakika ya 57 akizawadiwa kadi ya pili ya njano.

Nusu fainali ya pili, itachezwa baada ya wiki mbili zijazo.

error: Content is protected !!