Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Burudika Man Mo; Mkali aliyetajwa na Hayati Magufuli mkutanoni
Burudika

Man Mo; Mkali aliyetajwa na Hayati Magufuli mkutanoni

Spread the love

KILA mtu ana kipaji chake alichozaliwa nacho hapa duniani. Shida tunayokutana nayo ni namna ya kukivumbua kipaji hicho ili kiwe sehemu ya maisha yako.

Bahati mbaya, kipaji chochote hakiwezi kugeuka fursa, kama hutaweza kukihangaikia kwanamna moja ama nyingine. Unaweza kusota, lakini ukaja kusahau msoto huo.

Vipi kuhusu Diamond Platnumz. Anaukumbuka msoto wake? Ongeza na wakali wengine kama Ali Kiba, Konde Boy na wengineo wote kwa kiasi kikubwa walisota sana.
Miongoni mwa wasanii ambao nao wapo kwenye msoto wa kuyafikia mafanikio yake ni Maneno Mohamed ‘Man Mo’. Man Mo mwenye sauti tamu inayochagizwa na uwezo wake wa kuandika mashairi mazuri, anakumbuka jinsi Hayati Rais John Pombe Magufuli alivyosimama hadharani wilayani Kisarawe, mkoani Pwani na kumsifia kutokana na wimbo wake mzuri wa ‘Sweet Kitunguu’.

Akizungumzia mafanikio ya kutajwa na Rais wa nchi, Man Mo anasema hawezi kusahau tukio hilo katika maisha yake kwa kutajwa na mtu mzito anayeangaliwa na wengi.

“Sina mafanikio makubwa, lakini angalau naweza kusimama na kusema kazi yangu ilikuwa kati ya zile zinazomkosha Rais wa nchi.

“Hii inanifanya nisikate tamaa, niendelee na mapambano kwa sababu najua maisha ya sanaa yanahitaji moyo na kufanya kazi bila kuchoka kadri unavyoungwa mkono na wadau mbalimbali wa sanaa nchini,” Alisema Mo.
Mo anayetajwa kama moja ya wasanii wanaoweza kuandika vizuri maisha, anakumbuka kwa mara ya kwanza alivyoweza kuandika wimbo mzuri wa Nasimama ulioimbwa na mkali Lady JayDee.

Kama wengine, Mo alianza kuangalia kwanza sanaa ya mama yake marehemu Salma Musa Kaduga kabla ya kuanza kujiingiza kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva nchini.

“Mama kwangu alikuwa mtu wa kwanza kumuona na kutamani kuingia kwenye muziki, licha ya kwamba alihusika na ngoma tu kwenye shughuli mbalimbali kijijini kwao,” Alisema.

Msanii huyo anawataja pia wakali wengine wanaofanya kazi nzuri ambao mpaka sasa anatafuta namna ya kufikia sehemu nzuri kama njia ya kutimiza ndoto zake.

Anautaja mwaka 2010 kuwa ndio alianza rasmi harakati zake za muziki kwa kuamua kuja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya muziki wa kizazi kipya, licha ya kuwa alijichanganya pia katika shughuli mbalimbali ili mkono uende kinywani.

Studio za Sharobaro zilichangia pia kumuweka katika hatua nzuri kimuziki na kuandika nyimbo nyingi kama vile ni
Binti wa Kibara, Binti wa Kimasai, Nasimama na nyinginezo.

Baadae akafika kwenye Studio za Classic Sound chini ya mtayarishaji wake Monagenster aliyempa nafasi mbalimbali. Hata wimbo wake Sweet Kitunguu ulitengenezea kwenye studio hiyo, akiwa chini ya utawala wake wa zamani ANE, (African Network Entertainment.

Mpaka sasa nyimbo za Man Mo zilizofanya vizuri ni ‘Tike, Mapenzi Kazi, Hamida na Sweet Kitunguu zilizofanya vizuri. Mo yupo mbioni kuachia wimbo wake mpya uitwao Faraja, akitengeneza chini ya mtayarishaji wake Abidady.

Mo alizaliwa kwenye familia ya watoto wanne, huku yeye akiwa wa kwanza kuzaliwa mwaka 1994 huko Kimange, wilayani Chalinze mkoani Pwani.

Man Mo anasema kuwa licha ya muziki kuwa na ushindani mkubwa, ila hawezi kukurudi nyuma, akitumia pia kama sehemu ya kumuenzi mama yake aliyefariki Dunia na kumfanya ajiweke kando kwenye muziki kwa muda mrefu.
Man Mo anawataka wasanii washirikiane ili muziki wao uende vizuri kuliko ilivyokuwa sasa ambapo wanashindwa kuelewana.

Anakumbuka jinsi alivyoshindwa kuwa na maelewano mazuri na baba yake kiasi cha kununiana, kisa anajihusisha na muziki.

Mwimbaji huyo mwenye ndoto kubwa anasema muziki umezidi kupiga hatua kutokana na juhudi za wasanii wenyewe wanaokwenda na mabadiliko, ikiwamo mbinu ya kutumia vizuri mitandao ya kijamii.

Kuhusu serikali, Man Mo anaitaka iendelee kushirikiana na wasanii wote sanjari na kuwatafutia upenyo katika muziki wa Dunia, bila kusahau kufanikisha wasanii wa ndani kutoka nje mara kwa mara ili wakaongeze wigo mkubwa katika sanaa yao, akisisitiza kuwa bila wasanii wa ndani kupata maonyesho ya Kimataifa muziki wao hautapiga hatua.

Huyo ndiye Man Mo, mmoja ya wasanii waliopokewa na msoto na mwenye ndoto lukuki za kisanaa. Licha kuwa alitamba kwa muda kiasi cha kutajwa na Rais, lakini alisimama mara baada ya kumpoteza mama yake.

“Kitendo cha kumpoteza mama yake kilimvuruga na kushindwa kabisa kuendelea na muziki hadi wakati huu nilipokubali matokeo na kuendelea na harakati zangu ambao sasa naelekea kuachia wimbo wangu na video yake iitwayo Faraja,” Alisema Man Mo.

Anawaomba wadau na mashabiki wake kuendelea kumuunga mkono ili aendelee kwenye hatua nzuri kwa sababu muziki kwake ndio anachopenda akiwa na nia pia ya kuufanya kibiashara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Burudika

Piga makofi kwa Mr. Eazi …achomoka na ‘The Evil Genius’

Spread the loveMAKOFI kwa Mr Eazi! Staa wa Afropop, Mr Eazi ameachia...

Burudika

Kishindo cha Afro B katika “Wo wo wo” akiwa na Rich the Kid&Rimzee

Spread the loveSTAA ambaye alitambulishwa na ngoma maarufu, Afrowave ‘Drogba’, Afro B,...

Burudika

Mr. Eazi aachia Advice ikiwa ni ujio wa albam mpya

Spread the loveSTAA wa muziki kutoka nchini Nigeria, Mr.Eazi ni gwiji linapokuja suala...

error: Content is protected !!