August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Man City yairudia rekodi yao mbovu

Spread the love

SAHAU kupoteza mchezo kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Manchester United na kutupwa nje kwenye Kombe la Ligi, lakini Manchester City haikufanikiwa kupiga shuti hata mmoja liliolenga lango kwa dakika zote 90 za mchezo huo.

Mara ya mwisho klabu hiyo kumaliza mchezo bila ya kupiga shuti lolote lililolenga lango ilikuwa mwaka 2012 walipocheza na Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Pamoja na kumiliki mchezo kwa asilimia zaidi ya 51, lakini Manchester City walishindwa kutengeneza nafasi za mabao tofauti na wapinzani wao waliotengeneza nafasi chache licha ya kutomiliki mpira kwa asilimia kubwa.

Kukosekana kwa Kevin De Bruyne na David Silva katika eneo la ushambuliaji kwa Manchester City katika mchezo wa jana kulichangia kutotengenea nafasi nyingi kutokana na wachezaji hawa kuwa na ubunifu wa kipekee.

Kwa matokeo hayo, Manchester United imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ambapo itakutana na West Ham United waliyoiondosha Chelsea kwa mabao 2-1, huku Arsenal dhidi ya Southampton na Liverpool itamenyana na Leeds United.

error: Content is protected !!