May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Man City bingwa mpya EPL

Spread the love

 

KLABU ya Manchester City imetangzwa kuwa bingwa mpya wa Ligi Kuu nchini England mara baada ya Manchester United kukubali kichapo cha mabao 2-1, mbele ya Leceister City na hivyo kushindwa kufikia pointi za Manchester City hata wakishinda michezo iliyobaki. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mara baada ya kupoteza mchezo huo Manchester United inasalia kwenye nafasi yake ya pili akiwa na pointi 70, huku Manchester City kwenye nafasi ya kwanza akiwa na pointi 80 wote wakisalia na michezo mitatu.

Huu unakuwa ubingwa wa tano kwa Manchester City huku mataji matatu wakitwaa chini ya Pep Guardiolla ambaye alijiunga na kikosi hiko 2016 akitokea klabu ya Bayern Munchen kutoka Ujerumani.

Man City imechukua ubingwa katika msimu wa 2011-12, 2013-14, 2017-18, 2018-19 na 2020-21.

 

 

 

 

 

 

 

error: Content is protected !!