MAMLAKA ya Sweden imemrejesha Jean Paul Micomyiza mjini Kigali mwenye umri wa miaka 50,raia wa Rwanda aliyekamatwa nchini Sweden mnamo Novemba mwaka 2020 ,kwa tuhuma za mauaji ya kimbari ambayo aliyatekeleza alipokua mwanafunzi wa chuo kikuu. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa … (endelea).
Kwamujibu wa taarifa kutoka nchini Rwanda inasema kuwa ,Paul Micomyiza alipokelewa Rwanda siku ya jumatano Aprili 2022 ,nakuipongeza Sweden kwa mchango wake mkubwa wa kupambana bila kujali.
Micomyiza alikamatwa nchini Sweden Novemba mwaka 2020, kwa hati ya kukamatwa ya Rwanda.
Hata hivyo Micomyiza alipoteza rufaa dhidi ya kurejeshwa kwake Desemba mwaka jana, pia ameishi Sweden kwa zaidi ya muongo mmoja .Anatuhumiwa kwa uhalifu wa mauaji ya kimbari kwa jukumu lake la kuwasaka na kuwatambua Watusi ili kulipiza kisasi, baada ya mauaji yaliyofanwa na watusi hao mwaka 1994,alipokua na umri wa mika 22.
Micomyiza hajazungumza lolote kuhusu mashtaka anayokabiliwa nayo nchini Rwanda.
Leave a comment