May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mamilioni yapigwa kituo mabasi mwendokasi – CAG

Spread the love

 

RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2019/2020, imebaini kituo cha mabasi cha yaendayo haraka cha Kariakoo, jijini Dar es Salaam, kujengwa tofauti na mchoro ulivyooneshwa. Anaripoti Matilda Peter, Dar es Salaam … (endelea).

Ripoti hiyo iliyoandaliwa na CAG, Charles Kichere imewasilishwa bungeni jana Alhamisi, tarehe 8 Aprili 2021.

Kichere amesema katika uchunguzi wake kwenye mradi huo”nilibaini kituo cha mabasi cha Kariakoo kutojengwa kama mchoro ulivyoonesha kwa kujenga fremu ya aina tofauti na iliyoidhinishwa.”

Amesema, hatua hiyo “imesababisha malipo ya ziada ya Sh.234.37 milioni. Baada ya kuhoji uhalali wa malipo ya ziada, mshauri elekezi alirudisha Sh.130.89 milion, kama sehemu ya malipo yaliyozidi na kuacha kiasi cha Sh.103.48 milioni ambacho hakijarejeshwa.”

“Aidha, nilibaini nguzo zilizojengwa kwenye kituo hicho, zilikuwa fupi kuliko kimo kilichotakiwa kwenye michoro ya usanifu na michoro ya kina na kusababisha malipo ya ziada ya Sh.91.14 milioni,” amesema

Amesema, baada ya ukaguzi huo, Sh.83.43 milioni kati ya Sh.91.14 milioni, zilirejeshwa na mkandarasi na kuacha kiasi cha Sh.7.71 milioni ambacho hakikurejeshwa.

error: Content is protected !!