March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mamia wajitokeza kuupokea mwili wa Ruge

Spread the love

MWILI wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba umewasili jioni ya leo terehe 1 Machi 2018 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA).Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Mwili wa Ruge umewasili  JNIA ukitokea nchini Afrika Kusini alikokuwa anapatiwa matibabu kabla ya kufikwa na umauti tarehe 27 Februari 2019.

Mamia ya watu wamejitokeza kuupokea mwili wa marehemu Ruge, kuanzia uwanja wa ndege huku wengine wakijipanga katika viunga mbalimbali vya barabara ambako mwili huo ulipitishwa, kwa ajili ya kuupokea mwili huo huku wengi wao wakitokwa na machozi kuonesha ishara ya kuumizwa na kifo chake.

Mwili huo umepitishwa katika maeneo ya Buguruni, Karume, Magomeni, Morocco Hotel, Sinza Kijiweni, bamaga, ITV, ofisi za Clouds Media Group, Kawe na Lugalo.

Miongoni mwa viongozi walioongoza watu katika kuupokea mwili wa Ruge ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, January Muungano, January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mwili huo unatarajiwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, kisha hapo kesho unatarajiwa kuagwa katika viwanja vya Karimjee.

error: Content is protected !!