Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Maelfu wajitokeza kuaga mwili wa Mkapa Dar
Habari MchanganyikoTangulizi

Maelfu wajitokeza kuaga mwili wa Mkapa Dar

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli anawaongoza waombolezaji kuaga Kitaifa mwili wa Hayati Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Shughuli hiyo tayari imeanza Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo viongozi mbalimbali wa ndani na nje, wamejitokeza kuaga mwili wa Mkapa aliyekuwa Rais wa Tanzania kwa miaka kumi mfululizo kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.

Mkapa aliyezaliwa tarehe 12 Novemba 1938 alifikwa na mauti Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam kwa mshituko wa moyo.

Mara baada ya shughuli ya kuagwa kumalizika leo Jumanne, mwili huo utasafirishwa kwenda kijijini kwake, Lupaso wilani Masasi Mkoa wa Mtwara kwa maziko yatakayofanyika kesho Jumatano.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria ni marais wastaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Mrisho Kikwete na Aman Abeid Karume, Rais mstaafu wa Zanizbar.

Pia, mawaziri, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, makatibu wakuu, wakurugenzi pamoja na viongozi wa dini.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema shughuli ya leo haitakuwa ndefu sana.

Amesema, wanatarajia ikifika saa 9 alasiri, mwili wa Mkapa uwe umefika Lupaso Mkoa wa Mtwara.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!