Monday , 26 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Mambosasa awatoa hofu wanyoa ‘viduku’
Habari Mchanganyiko

Mambosasa awatoa hofu wanyoa ‘viduku’

Spread the love

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekanusha taarifa kuhusu kukamata wanyoa viduku, wavaa vimini zinazoendelea kusambaa. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Kamanda Mambosasa ameyasema hayo leo ofisini kwake akizungumza na waandishi wa habari huku kukiwa na habari zilizochapishwa katika Gazeti la Nipashe lenye kichwa cha habari ‘Polisi yakamata wavaa vimini, kunyoa viduku’.

“Mwandishi huyu jana alikuwa ananiambia nina operation gani dhidi ya wanaovaa nguo fupi na nilimjibu wazi, nilieleza swala la nguo fupi inategemea wapi umevalia, sikuishia wapi nikasema nitashangaa kuona mtu anavaa nguo fupi katika maeneo ya staha.

Amesema, alichokisema ni kwamba kuna matendo mtu anaweza akayafanya ambayo ni kinyume cha maadili ya Mtanzania, ambapo hata yeye kama kamanda wa mkoa analiona lina machukizo lakini si rahisi kuwakamata watu wanaovaa hivyo, lakini wanaofanya ufuska kwa kujipatia mapato hilo ni kosa la jinai.

“Huu ni uzushi mwandishi amechukua maneno akaweka kinywani kwangu ili niyaseme akauze gazeti, amejikosesha heshima, kukaa koridoni, kukaa kichakani harafu ukatengeza story harafu ukaenda kuiuzia Gazeti ni kujikosesha heshima,…..yaliyoandikwa hayakusemwa na Jeshi la Polisi na ninamtaka arudi kwa watanzania aombe radhi ili kuondoa usumbufu unaojitokeza.

“Sikueleza kwamba kuna msako unaoendelea wa kukamata watu waliovaa nguo fupi ispokuwa nilichokisema kuna matendo mtu anaweza kuyafanya ambayo ni kinyume cha maadili ya Tanzania”.

Hivi karibuni gazeti hilo liliomba radhi kwa kuandika taarifa zilizoelezwa kuwa ni za uzushi kuhusu rais Magufuli na lilijifungia lenyewe kuchapa gazeti lake la ‘Nipashe Jumapili’ kwa muda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RC Geita awafunda wahitimu wapya GGML

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito kwa...

Habari Mchanganyiko

Biteko asisitiza umuhimu wa EREA sekta ya nishati

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Tembo aongoza migongano binadamu, wanyamapori

Spread the loveIMEELEZWA kuwa asilimia 80 ya migongano baina ya binadamu na...

Habari Mchanganyiko

“Watanzania tembeleeni vivutio vya utalii”

Spread the loveSHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limewataka Watanzania kujitokeza kutembelea...

error: Content is protected !!