February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mambo yameiva Buyungu

Spread the love

WAKAZI wa Jimbo la Buyungu lililoko Wilayani Kankonko mkoa wa Kigoma, wamejitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Wakazi hao wamejitokeza leo tarehe 12 Agosti, 2018 kumchagua mbunge wa jimbo hilo lililoachwa wazi kufuatia kifo cha Mwalimu Kasuku Bilago aliyekuwa mbunge wa Buyungu.

Wananchi hao walijitokeza kuanzia majira ya asubuhi ambapo kuanzia mida ya saa moja kamili asubuhi zoezi la upigaji kura lilianza.

Katika uchaguzi huo, mgombea wa CCM, Christopher Chiza anachuana vikali na mgombea wa Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA, Eliah Michael.PICHA -8

Uchaguzi wa Buyungu unakwenda sambamba na uchaguzi mdogo wa kata thelathini na sita (36) unaondelea maeneo mbalimba katika kata hizo zilizoko Tanzania Bara.

error: Content is protected !!