Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mambo yameharibika: CUF, Chadema, NCCR joto lapanda
Habari za SiasaTangulizi

Mambo yameharibika: CUF, Chadema, NCCR joto lapanda

Spread the love

MIKASA katika uchukuaji na urejeshaji fomu imetamalaki katika maeneo mbalimbali nchini, viongozi wa upinzani sasa wanaelekeza kilio cha kwa serikali. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Leo tarehe 6 Novemba 2019, Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), amemwomba Rais John Magufuli, kuhakikisha anazuia uhujumu unaofanywa na wasimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa, uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba 2019.

Kauli ya Prof. Lipumba inashabihiana na ile ya John Mrema, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi na Uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana tarehe 5 Novemba 2019, alipomwomba Rais Magufuli, kuingilia kati changamoto zilizojitokeza n ahata wagombea wa upinzani kuenguliwa.

Prof. Lipumba amesema, kuna tatizo kubwa katika uchukuaji na urudishaji fomu kwenye uchaguzi huo, na kwamba wagombea wa vyama vya upinzani wameenguliwa kwa kuhujumiwa.

Mwenyekiti huyo wa CUF, amemuomba Rais Magufuli aelekeze mamlaka husika, kuongeza muda wa siku 4, ili changamoto hiyo ifanyiwe kazi.

“Uchaguzi unasimamiwa na TAMISEMI na iko chini ya Rais, Rais aingilie kati, siku 4 ziongezwe na ofisi zote za wasimamizi zifunguliwe, ili wagombea wachukue fomu, wajaze na warudishe,” ameshauri Prof. Lipumba.

Kiongozi huyo wa CUF amesema, kitendo cha wagombea wa upinzani kuenguliwa, hakioneshi taswira nzuri, na pia, kinavunja uvumilivu wa wananchi.

“Uvumilivu una mipaka, ukiisha tutaingia kwenye matatizo,” amesema Prof. Lipumba na kwamba, changamoto hiyo ikiondolewa, wananchi watakuwa na imani na uchaguzi.

“Mambo haya yakifanyiwa kazi, itarejesha imani ya watu. Kwamba anaheshimu katiba na anaheshimu haki ya wananchikuchagua viongozi wanaowataka,” amesema Prof. Lipumba.

James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi amelalamika rafu zilinazofanywa na wasimamizi wa uchaguzi huo, amesema ‘zimepita kiwango.’

“Ona kwenye jimbo la Vunjo ninaloliongoza mimi, wagombea wetu wote wameenguliwa. Hii ni hatari kwa usalama wa taifa.

“Wagombea wetu wameenguliwa katika vijiji 60 kati ya 78, katika hili nimeiandikia serikali barua ya kulalamikia rafu hizi,” amesema Mbatia.

Akizungumza na wanahabari jana, Mrema alisema Chadema itachukua hatua za dharura kukabiliana na hujuma dhidi yake.

Hatua hizo ni pamoja na kuitisha mkutano wa dharura ambao utatangaza hatua nzito.

“Kwa kaunzia kesho (leo), tumekubaliana sekretarieti ya kamati kuu itakaa tutakutana, lakini pia leo (jana) jioni viongozi wakuu wanakutana kwa dharura.”

Miongoni mwa malalamiko makubwa kwenye hatua hii ya uchukuaji na urejeshaji fomu, baadhi ya wasiamamizi waligoma kufungua ofisi ili kutoa fomu hizo.

Pia, kukataa fomu kwa madai ya kujazwa vibaya, wagombea wa CCM kupewa fomu na kurejesha usiku, wagombea wao kupigwa na mgambo pia kuwekwa chini ya ulinzi sambamba na kunyang’anywa fomu.

Tayari Jijini Mwanza, baadhi ya mitaa ikiwamo Kanindo uliopo Kata ya Kishili, uliokuwa ukiongozwa na Chadema, majina yote ya wagombea wa chama hicho hayakuteuliwa isipokuwa wa CCM.

Angela Kavalambi, Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi huo alidai, wagombea wa upinzani wote  walikosea kujaza taarifa zilizotakiwa. Waliotemwa ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Kanindo, Ndalawa Masibuka (Chadema), anayetetea kiti hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!