
Samia Suluhu Hassan, akiapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
RAIS wa Jamhuri ya Muungano, Samia Suluhu Hassan, anakabiliwa na kibarua kigumu cha kujisafisha kwenye mioyo ya wananchi na jumuiya ya kimataifa, kufuatia utawala wake, kugubikwa na mambo matano, yanayoitia doa katika siku za hivi karibuni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Miongoni mwa yanayotajwa kuwa ni kasoro na ambazo zinapunguza matumaini ya wananchi, ni pamoja na uanzishwaji wa tozo mpya ya miamala ya simu za mkononi; kudorora kwa uhuru wa kujieleza kisiasa na kasi ya kushughulikia mchakato wa Katiba Mpya.
Kabla ya kuibuka kwa dosari hizo, ndani ya siku 100 Rais Samia, alipongezwa na watu mbalimbali, ikiwamo jumuiya za kimataifa, kwa hatua zake mbalimbali, ikiwamo mapambano dhidi ya Corona, ufufuaji wa uchumi kwa kuvutia wawekezaji na kurejesha vyombo vya habari vilivyofungiwa na kuruhusu uhuru wa kujieleza.
Kwa habari zaidi, soma gazeti la Raia Mwema la leo, Jumamosi – Mhariri.
More Stories
Mapacha walioungana vifua watenganishwa Muhimbili
Butiku ataka nguvu ielekezwe kwenye maendeleo ya wananchi kuliko vyama
Kigogo Bavicha mbaroni kwa tuhuma za makosa mtandao