May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mambo matano mchezo Simba na Yanga

Spread the love

 

LICHA ya kwenda sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa watani wa jadi, uliowakutanisha klabu za Simba na Yanga kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaa, Raia Mwema tunakusogezea mambo matano yalijitokeza kwenye mchezo huo uliovuta hisia za mashabiki wengi wa soka nchini. Anaripoti Kelvin Mwaipungu….(endelea)

Mchezo huo wa mkondo wa pili mzunguko wa 21,ulipigwa juzi Aprili 30 majira ya saa 11 jioni.

Inonga dhidi ya Mayele

Wachezaji hao wawili raia wa Jamhuri ya Congo, kwao ilikuwa ni Zaidi ya mechi, Henock Inonga beki wa kati wa klabu ya Simba alifanya kazi kubwa kuhakikisha mshambuliaji hatari wa klabu ya Yanga, Fiston Mayele kutokuwa hatari langoni mwao kiasi cha kupachika bao lolote kambani.

Kabla ya mchezo huo, Mayele alinukuliwa na vyombo vya habari na kusema kuwa kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara alikuwa na deni la timu mbili ambazo alikuwa hajazifunguka, ikiwemo Namungo FC ambayo alifanikiwa kuifunga kwenye mchezo uliopita ambao klabu yake ya Yanga ilibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Deni pekee lililokuwa limebaki kwa mshambuliaji huyo ni kuifunga klabu ya Simba, ambayo hakufanikiwa kufanya hivyo kwenye mchezo wa kwanza ambapo timu hizo zilitoka bila ya kufungana huku beki wa Simba Henock Inonga akifanya kazi kubwa kumzuia mshambuliaji huyo.

Kwenye mchezo wa juzi wawili hao walionekana kama kukamiana kiasi cha kutambia wakiwa uwanjani muda mfupi kabla ya mchezo kuanza, lakini mwisho wa siku Inonga aliibuka shujaa kwa mara nyingine kwa kufanikiwa kumzuia Mayele kuapchika bao.

Wachezaji Kufturu Uwanjani

 Ni moja ya tukio ambalo ni nadra kutokea katika michezo minghi ambayo imechezwa kwenye kipimndi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani, lakini ili lilikuwa tofauti na kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Simba kwa wachezaji sambamba na benchi la ufundi kupewa dakika moja ya kufungulia kwa baadhi ambalo walikuwa kwenye swaumu.

Ikumbukwe mchezo huo ulinza majira ya saa 11 jioni katika siku ya 28 ya mfungo wa mwezi wa Ramadhani, ilipofika dakika ya 70 kipindi cha pili cha mchezo majira ya saa 12 na dakika 25, mwamuzi wa kati Ramadhani Kayoko Alipuliza filimbi kwa kutoa mapumziko ya dakika moja.

Timu zote mbili zilifungulia kwa kutumia tende na maji kwa wachezaji ambao walikuwa wamefunga, kwa upande wa Simba wachezaji waliokuwa kwenye swaumu katika dakika 70, uwanjani ni, Aishi Manula na Mohammed Hussen.

Kwa upande wa Yanga ni mlinda mlango Djigui Diarra, Kibwana Shomary, Bakari Mwamnyeto, Khlaid Aucho, Feisal Salum, Saido Ntibanzokiza na Djuma Shabani.

Kibwana shomari dhidi ya Morison, Kibu Denis, Chama na Sakho.

 Kwenye mchezo huo moja ya kitu kilichovutia watu wengi ni uwezo uliooneshwa na mlizni wa kushoto wa klabu ya Yanga, Kibwana Shomari mara baada ya kuwakabili wachezaji wane wa klabu ya Simba kwa nyakati tofauti waliokuwa wakicheza upande wake.

Mwanzoni mwa mchezo huo Kibwanba alifanikiwa kumakabili vizuri BEnard Morison kiasi cha kushindwa kufurukuta kiasi cha kumfanya kocha wa Simba Pablo Franco Martini kumtoa kumfanyia mabadiliko katika kipindi cha pili cha mchezo na kuingia Kibu Denis ambaye nae hakufua dafu kwa mlinzi huyo mwenye umbo dogo.

Licha ya wachezaji hao wawili, kwa nyakati tofauti Clatous Chota Chama na Pape Ousmane Sakho walijaribu kwenda kucheza upande wa beki huyo na alifanikiwa kuwadhidi vizuri na pengione kumfanya kuwa mmoja ya mchezji alikuwa na mchezo muzri siku hiyo.

Waamuzi

Ni nadra sana kwenye miaka mingi kukuta mchezo wa Yanga dhidi ya Simba, ukamilizika bila kuwepo kwa lawama kwa waamuzi waliohusika kwenye mchezo huo, hali hiyo ilikuwa tofauti kwenye mchezo uliopita kwa waamuzi wanne wa mchezo huo kwa kufanikiwa kulimudu vizuri pambano hilo bila kutokea sintofahamu yoyote.

Mwamuzi wa kati kwenye mchezo huo alikuwa ni Ramadhan Kayoko kutokea Dar es Salaam, ambapo mpaka dakika 90 zinakamilika alionesha kadi sita za njano kwa ujumla tena kwenye matukio ambayo yalikuwa yanastaili adhabu hiyo.

Katika kadi hizo sita, nne zilikuwa upande wa Yanga ambazo alionesha kwa wachezaji Djigui Diarra, Kibwana Shomari, Jesus Moloko na Khalid Aucho, huku upande wa Simba zikitoka kadi mbili kwa Henock Inonga na Bernad Morison.

Waamuzi wengine walihusika kwenye mchezo huo ni Frank Komba Mwamuzi msaidizi namba moja kutoka Dar es Salaam, Mohammed Mkono mwamuzi msaidizi namba mbili kutoka Jijini Tanga, na Elly Sasii mwamuzi wa akiba kutoka Dar es Salaam.

Manula, Diarra kuwa likizo

 Ni mara chache sana kukuta mchezo mkubwa kama wa Simba na Yanga, kumalizika bila makipa kuokoa mipira ya hatari (saves), kutokana na ukubwa wa timu na ubora wa wachezaji waliokuwepo.

Kwenye mchezo huo, Mlinda mlango wa klabu ya Simba Aishi Manula hakufanikiwa kupigiwa hata shuti moja lililolenga lango lake (On Target), licha ya muda mchache kwenye mchezo huo Yanga kuonekana kuleta kashikashi kwenye lango la Simba.

Kwa upande wa Diarra katika dakika 90 za mchezo alidaka mipira miwili ambayo pia haikuwa hatai kiasi cha kumsumbua kwenye lango hilo kutokana na safu yake ya ulinzi kufanya kazi kubwa.

error: Content is protected !!