July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mambo matano makubwa mchezo Simba na Yanga

Rais Samia Suluhu Hassan (kushoto) akishuhudia mchezo kati ya Simba na Yanga

Spread the love

 

MARA baada ya kufanyika kwa mchezo mkubwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kati ya Simba ambao walikuwa wenyeji mbele ya Yanga na kupoteza mchezo huo kwa bao 1-0, mechi hiyo ilikugubikwa na matukio mbalimbali kabla na baada ya dakika 90 za mchezo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo namba 208, ulichezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar es Salaam majira ya saa 11 jioni, na Yanga kumaliza shughuli hiyo ndani ya dakika 11, kwa kupata bao la kwanza na la ushindi kupitia kwa kiungo wake Zawadi Mauya.

Kama ilivyo ada, mchezo unapokutanisha timu hizo mbili, huwa haukosi matukio ndani na nje ya uwanja kutokana na ukubwa wa timu hizo mbili.

Ukiachana na matokeo tukio la kwanza kubwa kwenye mchezo huo, ni ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kushudia mchezo huo, kwa mara ya kwanza toka alipoapishwa kuwa rais tarehe 19 Machi, 2021

Rais Samia alichukua nafasi hiyo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dk. John Magufuli.

Hayati Magufuli alifariki tarehe 17 Machi, kwenye Hospitali ya Mzena, jijini Dar es Salaam kufuatiwa kuugua maradhi ya mfumo wa umeme wa moyo.

Rais Samia alikuja kushuhudia mchezo huo kwa mara ya kwanza toka achukue wadhifa huo, ambapo aliingia uwanjani hapo majira ya saa 10:55, na kushuhudia Yanga ikiondoka na pointi tatu, katika dakika 90 za mchezo.

Tukio hilo liliwavutia maelfu ya mashabiki waliojitokeza kwenye mchezo huo, kiasi cha kumshangilia mara baada ya kutinga uwanjani hapo kwa kushtukiza.

Hii itakuwa mara ya pili kwa Marais wawili tofauti, kuhudhulia mchezo wa watani wa jadi (Simba na Yanga), katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi minne.

Hayati Rais Magufuli alifanikiwa kuhudhulia mchezo wa watani huo wa jadi kwenye msimu uliopita, tarehe 8 Machi, 2020, kwenye huo huo, ambapo pia Yanga waliondoka na ushindi wa bao 1-0, lilofungwa na Bernard Morrison.

Tukio la pili na kuvutia kwenye mchezo, lilitokea kwa mwamuzi msaidizi namba moja, Frank Komba, kutoka Dar es Salaam, alipojikuta ndani ya kiwanja badala ya kuwa kwenye mstali, akikimbizana na kasi ya mpira alikuwa nao kiungo wa Simba, Claytous Chama, kwenye dakika 35 ya mchezo, wakati Simba walipofanya shambulizi la kushtukiza (counter Attack), langoni kwa Yanga.

Yanga nao hawakuwa nyuma kwenye kwenye matukio hayo, ambapo tukio namba tatu lilifanywa na klabu ya Yanga ambapo ni nje ya utaratibu mara baada ya kuamua kupitisha basi lilibeba wachezaji kwenye geti dogo la Uwanja wa Uhuru, badala ya kutumia geti kubwa la uwanja huo.

Kikosi hiko kilifika uwanjani majira ya saa 9 jioni na kupitisha gari lao, kwenye geti la uwanja mdogo wa Uhuru kinyume na utaratibu wa kanuni za mashindano.

Tukio linguine kwenye kikosi cha Yanga, ni mara baada ya kutotumia mlango mkubwa wa kuingia uwanjani kwenye eneo la kuchezea (pitch), wakati wa kwenda kupasha misuli moto kabla ya mchezo na kuamua kupita kwenye mlango wa pembeni.

Kikosi hiko pia cha Yanga hakikuishia kufanya hivyo, bali baada ya wachezaji kushuka kwenye gari hawakuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vilivyopangwa na kuamua kukaa nje ya vyumba hivyo, kinyume na utaratibu wa kanuni za mashindano.

error: Content is protected !!