October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mama wa Kabendera afariki dunia

Spread the love

VERDIANA Mjwahuzi, Mama wa Erick Kabendera, Mwanahabari aliyeko mahabusu akituhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, amefariki dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa ya kifo hicho imetolewa na Familia ya Kabendera,  leo tarehe 31 Desemba 2019.

Kwa mujibu wa familia ya Kabendera, Mama Verdiana amefariki dunia Jumanne ya leo tarehe 31 Desemba 2019, katika Hospitali ya Amana, jijini Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu.

Wiki mbili kabla ya kifo chake, Mama Verdiana alimuomba Rais John Magufuli kumsamehe mwanaye Kabendera na kumuacha huru, kwa kuwa ndiye msaada na nguzo kwa familia yake.

Mnamo tarehe 13 Desemba 2019 akiwa jijini Dar es Salaam, Marehemu Verdiana aliwaeleza wanahabari kuwa, Kabendera alikuwa anamsaidia kumpa fedha za matibabu, lakini tangu mwanaye huyo alipokamatwa, amekuwa akikosa huduma hiyo muhimu, ikiwemo kutopata dawa kwa wakati.

Kabendera yuko katika Mahabusu ya Gereza la Segerea, tangu alipokamatwa mwezi Julai mwaka huu, akituhumiwa kwa makosa ya Utakatishaji fedha, kukwepa kodi pamoja na kuongoza kikundi cha uhalifu.

error: Content is protected !!