Friday , 9 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mama Samia: Watanzania ni hodari kutengeneza sera, si kuzitumia
Habari za Siasa

Mama Samia: Watanzania ni hodari kutengeneza sera, si kuzitumia

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hasani amesema, Watanzania ni mahodari kutengeneza sera, sheria na kanuni lakini siyo watekelezaji. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Ametoa kauli hiyo leo 31 Julai 2019 kwenye kongamano la ufunguzi wa jukwaa kuhusu ‘usimamizi bora wa misitu kwa upatikanaji wa rasilimali maji endelevu”’iliyofanyika jijini Dodoma chini ya Taasisi ya Uongozi.

Katika kongamano hilo Mama Samia amesema, Tanzania imekuwa na wataalamu wengi wenye kujua kuelezea mipango, sara, kanuni na sheria viziri katika makongamano ya kitaifa hivyo kupewa pesa za utunzaji, lakini utekelezaji duni.

Kutokana na hali hiyo amesema, umefika wakati wa kufanya kazi kwa vitendo na siyo kukaa ofisini na vikao kwa lengo la kuhesabiana posho.

Mbali na hilo amesema, takwimu za mwaka 2015 zilizotolewa na Maliasili na Utalii zinaonesha, Tanzania imepoteza heka 372,816.

Na kuwa, uharibifu huo unatokana na shughuli za kibinadamu kuwa nyingi hasa katika misitu isiyokuwa na usimamizi wa kisheria.

Amesema, takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine mkoani Morogoro mwaka 2017, kiwango cha kutoweka misitu kimefikia hekta 469,420 kwa mwaka.

“Hili ni sawa na ongezeko la hekta takribani 100,000 ndani ya miaka miwili, hali hii siyo rafiki kwa upatikanaji endelevu wa rasilimali maji,” amesema.

Amesema, kukosekana kwa misitu kunasababisa kuchelewa kwa maendeleo ya nchi.

Akizungumzia uharibifu wa mazingira amesema, hakuna siku ambayo moyo wake uliumia alipoona wanyama wakipanga foleni kunywa maji.

“Kuna siku niliumia sana maana niliona jambo la ajabu ambalo sijawabi kuliona duniani. Jambo hilo ni pale nilipokuwa Ruaha na kuona wanyama wakipanga foleni kunywa maji huku wakimtegemea  Tempo awe ndiye anayechimba shimo maji yatoke ili wayapate,” amesema Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!