May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mama Samia: Ni wakati muhimu Watanzania tushikamane

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema, hakuna kipindi ambacho taifa hilo, lipanaswa kujenga umoja, kama kipindi hiki cha sasa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Amesema, ni kawaida mwanadamu kukaguliwa kaguliwa na kwamba ni muhimu kwa wananchi, kutosikiliza maneno kutoka nje ya Taifa hilo, lililopo Afrika Mashariki.

Amesema, “Tanzania tuko salama. Nikawaida ya mwanadamu kukaguliwa kaguliwa, mara mafua, mara homa, mara chochote kile. Niwaombe dua zenu, ili tuendelee kuwa salama,” amesema Mama Samia

Mama Samia ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, tarehe 15 Machi 2021, wakati akizungumza na wananchi mkoani Tanga. Kiongozi huyo wa pili kitaifa, aliwasili mkoani humo leo asubuhi kwa ziara rasmi ya kiserikali.

Makamu huyo wa rais, hakutaja yule anayekaguliwa mwili wake. Hakusema nani anayeumwa mafua, anayeumwa homa au ugonjwa mwingine na ambaye taifa hilo.

Akisitiza hoja yake ya kuwapo umoja wa kitaifa, Mama Samia amesema, “lakini nataka niwaambie kwamba, katika wakati muhimu wa Watanzania kushikamana, ni wakati huu.”

Amesema, “huu ndio wakati wa kujenga umoja. Huu siyo wakati wa kusikiliza maneno kutoka nje, nasi yakatupaganya vichwa. Ninawaomba wote tushikamane kwa umoja kama Watanzania. Tufanye kazi, ili taifa letu lipate kusonga mbele.”

Mama Samia amesema, tusimame na tushirikiane ili taifa letu liweze kusogea. Uimara wa taifa, utaleta maendeleo.

Amesema, miradi inayotekelezwa kama afya na elimu, iko ndani ya ilani ya uchaguzi au rais alipita na kutoa ahadi.

Makamu hiyo wa wa rais, awali alianza kwa kuweka jiwe la msingi katika Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya Halmashauri ya Handeni na baadaye kufungua kiwanda cha cha Nafaka, kilichojengwa Mchungwani.

Akiwa katika eneo la Kabuka, kiongozi huyo amesema, Tanzania imefanya vizuri katika ujenzi wa uchumi wake na hivyo kuwa nchi ya 10 duniani ambayo uchumi wake unaku.

“Nilikuwa naangalia taaifa za dunia, Tanzania sasa ndio iko namba 10 katika kukua kwa uchumi,” amesema.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!