May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mama Samia kuapishwa leo

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

LEO Ijumaa saa 4:00 asubuhi, tarehe 19 Machi 2021, Ikulu ya Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ataapishwa kuwa Rais wa sita wa Tanzania katika awamu ya tano. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Mama Samia anaapishwa kuhitimisha awamu ya tano ya uongozi wa miaka minne na ushehe iliyosalia, baada ya Rais John Pombe Magufuli (61), kufariki dunia.

Rais Magufuli alifariki dunia Jumatano ya tarehe 17 Machi 2021 katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu ya mfumo wa umeme wa moyo.

Mama Samia, mwenye umri wa miaka 61, anatarajiwa mara baada ya kumaliza kuapishwa, kutangaza ratiba ya mazishi ya Rais Magufuli ambaye atazikwa nyumbani kwao Chato mkoani Geita.

error: Content is protected !!