Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari Mama Samia atoa wito uibuaaji fursa
Habari

Mama Samia atoa wito uibuaaji fursa

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

WAWEKEZAJI na wafanyabiashara nchini wameshauri wa kuibua fursa zinazofungamana na sekta ya madini ili ajili kukuza uchumi wa Taifa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumatatu tarehe 22 Februari 2021 na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassani wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini Tanzania, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Mama Samia amewaomba washiriki wa mkutano huo, kujadili namna ya kuifanya sekta hiyo izidi kukuza uchumi wa nchi.

“Natarajia  kongamano hili litaibua fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya madini zenye mafungamano na sekta nyingine, mkajaidli  jinsi ya kuibua mambo yatakayofanywa na sekta ya madini lakini yatafungamana na sekta ya biashara na nyingine zinazoendana na sekta ya madini,” amesema Mama Samia.

Amewataka washiriki wa mkutano huo, kueleza changamoto wanazokutana nazo katika sekta ya madini ili zifanyiwe kazi na serikali. Huku akiwahimiza kufuata sheria za nchi katika utekelezaji wa shughuli zao.

Hata hivyo, Mama Samia amesema sekta ya madini imeendelea kutoa mchango mkubwa katika mapato ya nchi, na kwamba fedha zilizokusanywa kutokana na shughuli za madini zimekuwa zikiongezeka katika miaka mitano mfululizo, kuanzia mwaka wa fedha wa 2015/2016 hadi 2019/2020.

“Mwaka huu wa fedha 2020/21, wizara ya madini imepangiwa kukusanywa  Sh. 526.7 Bil. ambayo ni sawa na wastani wa Sh.  43.89 Bil. kwa mwezi.  Takwimu zinaonesha kuwa kipindi cha Julai 2020 hadi Januari 20 21, wizara imekusanya Sh. 360.74 Bil. sawa na asilimia 117 ya lengo la kipindi hiki,” amesema Mama Samia.

“Pamoja na ufanisi huo, mwenendo wa ukusanyaji maduhuli katika kipindi cha miaka mitano imekwenda kwa kukuwa, maduhuli yameongezeka kukusanywa kutoka 2015/2016 hadi 2019/sh. 270 bilioni zilikusanywa  2015/2016 sh 528 bilioni zilikusanywa 2019/2020. Mnaweza kuona ukuaji wa sekta ya madini,” amesema Mama Samia.

Amesema serikali imepanga hadi kufikia 2025, sekta ya madini ichangie asilimie 10 ya pato la taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!