May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mama Samia: Amani inatokana na haki

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

MAMA Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Tanzania amesema, amani inatokana na haki. Anaripoti Brightness Boaz … (endelea).

Akizungumza wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) leo tarehe 24 Januari 2021, jijini Mwanza amesema, haki ndio msingi wa amani.

Mheshimiwa Jaji Mkuu sote unatambua kuwa kuendelea kwa taifa lolote, kiuchumi, siasa na kijani inategemea amani na utulivu uliopo katika jamii husika. 

“…amani ya kweli sio kutokuwepo na fukuto, migogoro na mivutano, bali ni uwepo wa haki ambayo itazuia hayo yote, na hilo ndilo jukumu la mahakama.”

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma; Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dk. Eliezer Mbuki Feleshi, umewakutanisha wanachama wake zaidi ya 200.

Miongoni mwa wanachama hao ni Majaji wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu, Wasajili, Naibu Wasajili, Mahakimu na maofisa wengine wa mahakama katika ngazi mbalimbali.

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma

Mama Samia amesema, haki ni mojawapo ya misingi mikuu ya kuleta amani katika taifa lolote duniani, hivyo haki ikitolewa kwa wakati, itaongeza maendeleo kwa haraka, na pia ikicheleweshwa, huchelewesha maendeleo. 

“Lakini ucheleweshaji huo husababisha migogoro inayopelekea kuvurugika kwa amani, utulivu na kupelekea watu kutoweza kuishi vizuri,” amesema.

Amesema, Mahakama Kuu ilianza na majani watatu, Jaji Mkuu na majaji wawili, baada ya mageuzi na mapito mengi, kwa sasa Mahakama Kuu ina majaji wanawake 23 na wanaume 50.

Na kwamba, kwa sasa kuna majaji wa rufani, wanawake saba na wanaume tisa “nataka nipongeze sana hatua hii  iliyofikia, ilikua ni ndoto kuona mwanamke anasimama kama jaji wa mahakama ya rufani au jaji wa mahakama kuu, lakini kwa mageuzi mbalimbali, mifumo ya elimu na mambo yaliyotokea, sasa imewezekana.”

Amesema, katika kipindi cha miaka 100, mahakama imepitia mapito mengi kutoka kuwa chombo cha kikoloni mpaka kuwa chombo huru na kwamba, mahakama imeweza kuhimili mabadiliko mbalimbali ya kikanda na kimataifa.

“Hakika hii ni safari ndefu sana, iliyojaa mabonde na milima lakini hatimaye mmevuka na kufika hapa mlipo katika Karne ya 21, mkikabiliana na yanayotokana na wimbi la mapinduzi ya nne ya viwanda,” amesema.

error: Content is protected !!