October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mama Salma Kikwete ajitosa ubunge Mchinga

Spread the love

MAMA Salma, Mke wa Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amechukua fomu kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge Mchinga Mkoa wa Lindi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mama Salma amechukua fomu hizo leo Jumatano tarehe 15 Julai 2020 kuwania jimbo hilo ambalo lilikuwa likiongozwa na Hamidu Bobali wa Chama Cha Wananchi (CUF).

Mama Salma alikuwa mbunge wa kuteuliwa na Rais John Pombe Magufuli kuanzia tarehe 1 Machi 2017.

Katika hatua nyingine, : Mtangazaji na Mtayarishaji wa vipindi Clouds Media Group, Kijakazi Yunus (Binti Lindi) amechukua fomu kuomba ridhaa kugombea ubunge viti maalum kupitia kundi la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Lindi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

error: Content is protected !!