December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mama Salma atangazia neema wanawake

Wanawake wakisherehekea siku ya Wanawake Duniani

Spread the love

SALMA Kikwete, mke wa Rais wa Jamhuri, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amewataka wanawake kutumia alichoita, “fursa za kiuchumi,”ili kuondokana na umasikini. Anaandika Pendo Omary… (endelea).

Akizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya wanawake duniani mkoani Dar es Salaam, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Salma amesema, “pamoja na mafanikio ya wanawake nchini, maadhimisho haya ni sehemu ya mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazowakabali.”

Kauli mbiu ya maazimisho ya mwaka huu ni Uwekezaji Wanawake. Amewataka wanawake nchini; kutekeleza kauli mbiu hiyo kwa vitendo.

Mama Salma amesema, mkoa wa Dar es Salaam pekee kwa mwaka wa fedha 2014/2015 ulitenga Sh. 1.05 bilioni ili kuhakikisha wanawake wanapata mikopo ambayo itawasaidia kuondokana na umasikini.

Kwa mujibu wa Mama Salma, fedha hizo ziligawanywa kwa Halmashauri tatu za jiji la Dar es Salaam za Ilala, Temeke na Kinondoni.

 Manispaa ya Ilala ilipata Sh. 500 milioni, Kinondoni Sh. 250 milioni na Temeke Sh. 300 milioni.

Amedai kuwa fedha hizo bado zipo na amewaomba wanawake kujitokeza kuziomba ili ziwasaidie kwa ajili ya mikopo.

Aidha, Mama Kikwete amesema, wanawake wanapaswa kujikita katika ujasiliamalia na kushiriki katika vikundi vya kuweka na kukopa ikiwa ni sehemu ya kufikia mafanikio makubwa ya kibiashara.

Mbali na umasikini, mke huyo wa rais ambaye alikuwa masikini wa kutupwa na sasa amekubuhu kwa utajiri amezitaja changamoto zinazowakabili wanawake kuwa ndoa za utotoni, uzazi salama, ukatili wa kijinsia, mfunmo ndume, ubaguzi na mimba za utotoni.

error: Content is protected !!