July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mama na Baba Lishe waanzisha Saccos

Spread the love

JUMUIYA ya Mama lishe na baba lishe Mkoa wa Dar es Salaam, wameanzisha ‘Mama na Baba Lishe Saccos’ kwa lengo la kutafuta ufumbuzi na kujitatulia mahitaji mbalimbali ya kimaendeleo. Anaandjika Hamisi Mguta … (endelea).

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mama na Baba Lishe, Ramadhani Mhonzu amesema kutokana na mama na baba lishe kuwa wengi katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na manispaa nyingine nchini wameamua kutafuta ufumbuzi na kujitatulia mahitaji kwa kufungua Mama na Baba Lishe Saccos.

Mhonzu amesema Mama na Baba Lishe wanakumbwa na tatizo la ukosefu wa mitaji inayopelekea kukosa mikopo, sasa wameamua kujitambua dhidi ya kutatua matatizo hayo.

Amesema kuwa wanaamini chombo hicho kilichoanzishwa kitaweza kusaidia na kuratibu maendeleo yao wakiwa ni watu muhimu na watoa huduma za vyakula kwa watu wa nyanja zote.

Mratibu katika Jumuiya hiyo, Saidi Mohamed amesema mfumo huo utawezesha kutambulika na kukuza jamiii kwa jumuiya ya Mama na Baba lishe, ambapo watatambulika katika taasisi mbalimbali za kifedha.

Saccos hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya Jumapili ambapo kutakutanishwa Mama na Baba Lishe katika ukumbi wa PTA Sabasaba viwanja vya mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kukutanisha Mama na Baba Lishe itakayotoa mafunzo ya usafi wa mazingira.

Katibu wa Mama Lishe katika soko la Ilala, Jane Nyanda amesema wamekuwa na changamoto kwa muda mrefu ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia ambao umekuwa ukiungamana na kushuka uchumi katika biashara zao.

“Tunapigwa na kudhurumiwa na wateja pamoja na kunyanyaswa kutokana na kuwa Mama lishe wengi tunafanya kazi pasipo na misingi yao binafsi mwisho wake kujikuta wakifanyabiashara bila kuwa na kipato,” amesema Nyanda.

error: Content is protected !!