May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mama mzazi wa IGP Sirro afariki dunia

Spread the love

MONICA Nyabyamari, mama mzazi wa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) wa Tanzania, Simon Sirro, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumamosi, tarehe 10 Aprili 2021, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea).

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime imesema, msiba uko nyumbani kwa IGP Sirro, Masaki mkoani Dar es Salaam, karibu kwa Hayati Rais Benjamin Mkapa.

Misime amesema, taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika nyumbani kwa marehemu, Kijiji Kiabakari, Butiama mkoani Mara.

error: Content is protected !!