Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mama Mkapa awezesha wanawake kupata Sh trilioni 11
Habari za SiasaTangulizi

Mama Mkapa awezesha wanawake kupata Sh trilioni 11

Mama Anna Mkapa
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Mfuko wa Fursa sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa ambaye pia ni mke wa Hayati Rais Benjamin Mkapa amesema tangu kuasisiwa kwa mfuko huo miaka 25 iliyopita, wanawake wajasiriamali wameuza ndani na nje ya nchi bidhaa zenye thamani ya Sh trilioni 11 na oda za Sh bilioni 694.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya EOTF kuwezesha kupatikana kwa masoko ya bidhaa za wanawake wajasiriamali na vijana kupitia maonesho mbalimbali yanayoratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mama Mkapa ametoa kauli hiyo leotarehe 27 Juni, 2022 jijini Dar es Salaam katika Sherehe za maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa Fursa sawa kwa wote ambazo pia zimehudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema kwa miaka 25 EOTF iligawanya majukumu yake katika program tatu, ya kwanza ikiwa ni Women In Poverty Eradication (WIPE) ambayo ni maarufu kwa kuwajenga na kuwawezesha wanawake na vijana wajasiriamali uwezo wa kujikomboa kiuchumi kutokana na kazi zao za kila siku.

“Kwa miaka 25 tumetoa mafunzo ya ujasiriamali na stadi za biashara kwa wanawake wajasiriamali wapato 6000 waliozalisha ajira zaidi ya 25,000 na kuanzishwa viwanda vidogovidogo.

“Programu ya pili ambayo ni Education Support, imesaidia jamii maskini ufadhili wa kuwawezesha watoto 1,755 kutoka shule ya chekechea, msingi, sekondari, VETA hadi vyuo vikuu ndani na nje ya nchi.

“Waliohitimu sasa wanatumikia Taifa, kuna walimu, madaktari, wanasheria, wanadiplomasia, viongozi wahasibu fani nyingine, amesema.

Aidha, amesema EOTF pia imesaidia ujenzi na ukarabati wa shule, kugawa vitabu vya kufundishia na kusoma zaidi ya milioni kwa shule na vyuo, uchimbaji wa visima vya maji salama na ugawaji wa viti mwendo kwa wanafunzi walemavu na madawati.

“Programu ya tatu ni Health support, iliwalenga akina mama na watoto katika elimu ya uzazi na maradhi hatarishi kama kansa, malaria, Ukimwi, Uviko -19, ujenzi wa wodi ya wazazi, watoto, nyumba ya kuhifadhi maiti, ukarabati wa zahanati, vifaa mbalimbali za hospitali na n k.

Rais Samia Suluhu Hassan

“Pia ujenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima, cha Kibaha Children Center mkoani Pwani ambacho kinatoa huduma zote kama mzazi kwani tumejenga shule kwa ajili ya watoto na wale wanaoishi jirani na zahanati ya kisasa kwa matumizi ya kituo na majirani,” amesema.

Pamoja na mambo mengine amesema Mfuko huo unakabiliwa na changamoto ya kuhudumia makundi maalumu, uhaba wa watumishi na vifaa tiba kwa zahanati ya kituo cha Kibaha.

Pia amesema wanakabiliwa na changamoto ya eneo na fedha za kujenga Kituo cha Kibiashara cha Wanawake kitakachotoa mafunzo mbalimbali ya kuboresha bidhaa na kutumia teknolojia rafiki na kuweka bidhaa zao kwa ajili ya mauzo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!