Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mama mbaroni kwa mauaji ya mwanaye
Habari Mchanganyiko

Mama mbaroni kwa mauaji ya mwanaye

Spread the love

 

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia Latifa Bakari (33), mkazi wa Mabibo, kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wa mdogo wake (2), aliyekabidhiwa kwa ajili ya kumlea. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa mapema leo, tarehe 12 Aprili 2022 na Kamanda wa Jeshi la Polisi wa kanda hiyo, ACP Jumanne Muliro.

Kamanda Muliro amesema, mtuhumiwa alifanya tukio hilo tarehe 5 Aprili mwaka huu, baada ya kumpiga kupita kiasi mtoto huyo, kisha tarehe 6 Aprili 2022, aliuchukua mwili wake kisha akaenda kuutupa maeneo ya River Side, Ubungo, jijini humo.

“Baada ya kubaini kuwa mtoto huyo amefariki baada ya kipigo, tarehe 12 Aprili 2022, mtuhumiwa aliuchukua mwili wa mtoto, kuukunja, kuuweka kwenye ndoo ya plastiki, kisha kuudumbukiza kwenye kiroba na kwenda kuutupa eneo la River Side UBUNGO,” amedai Kamanda Muliro.

Kamanda Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro

Kamanda Muliro amesema, Jeshi la Polisi lilipata taarifa ya tukio hilo kutoka kwa majirani wa mtuhumiwa huyo, ambao waliitoa baada ya kutomuona mtoto.

“Baada ya majirani kutomuona mtoto huyo kama ambavyo si kawaida, walitoa taarifa Polisi, Polisi ilimuhoji kwa kina mtuhumiwa akakiri mauaji hayo na kwenda kuwaonesha Polisi mwili wa mtoto huyo ulipokuwa,” amedai Kamanda Muliro na kuongeza:

“Mwili huo umepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo baada ya mifumo ya kisheria kukamilika.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!