August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mama lishe wapigiwa chapuo

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu akizungumza na baadhi ya Mama Lishe wa soko la Feri, Dar es Salaam

Spread the love

UMMY Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto ameshauri halmashauri zote nchini kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya mama lishe, anaandika Happiness Lidwino.

Waziri Ummy amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Taasisi ya Basilla Mwanuku yenye lengo la kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo amesema, anatambua umuhimu wa mama lishe kwani wana mchango mkubwa katika jamii hivyo angependa kuona wanaheshimiwa na kuendelezwa kama wafanyabiashara wengine.

Amesema, Manispaa ya Ilala na Kinondoni zina zaidi ya mama lishe 19,500 ambapo kati yao asilimia 96 wanafanya kazi hiyo katika mazingira magumu.

Na kwamba wanakutana na matatizo mbalimbali ikiwamo ukosefu wa mitaji,vitendea kazi, mazingira duni na utunzaji wa kumbukumbu.

“Tunahamasisha kampuni binafsi kuchangia kina mama lishe kwa kuwapatia vifaa vitakavyowawezesha kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa,” amesema Ummy.

Mwanukuzi, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo baada ya kufanya utafiti kwa muda mrefu na kuzungumza na mama lishe amesema waligundua kuna matatizo mengi yanayowasibu.

“Nusu ya nguvu kazi ya Taifa inalishwa na kina mama lishe hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuwasaidia kujiinua kiuchumi ” amesema Mwanukuzi.

Amesema ataanzisha semina kwa kila kata ili kutoa elimu juu ya kufanya kazi katika mazingira safi na salama kwa ajili ya kuimarisha na kulinda afya za walaji.

error: Content is protected !!