May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mama Kikwete afariki dunia

Nuru Khalfan Kikwete, mama mlezi wa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spread the love

NURU Khalfan Kikwete, mama mlezi wa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefariki dunia mapema hii leo, anaandika Pendo Omary.

Bi. Nuru amefariki mapema leo asubuhi katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa akisumbuliwa na maradhi yanayohusiana na uzee.

Taarifa ya kufariki kwa mlezi huyo wa Dk. Kikwete imetolewa na Ridhiwani Kikwete, Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambye pia ni mtoto mkubwa wa rais huyo mstaafu.

Ridhiwani ameandika katika ukurasa wake wa Facebook na Twitter , “Tanzia ndugu na marafiki. Nasikitika kuwatangazia msiba/kifo cha bibi yetu Bi. Nuru Khalfan.”

error: Content is protected !!