May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mama Janeth akabidhiwa bendera ya Tanzania

Spread the love

 

JANETH, Mjane wa aliyekuwa Rais wa Tanania, John Pombe Joseph Magufuli, amekabidhiwa bendera ya Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Chato … (endelea).

Bendera hiyo amekabidhiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ), leo Ijumaa tarehe 26 Machi 2021, mara baada ya jeshi, kumaliza kuuzika mwili wa Dk. Magufuli

Makabidhiano hayo yamefanyika mbele ya kaburi la Dk. Magufuli, nyumbani kwao Chato mkoani Geita na kuongozwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

“Kwa niaba ya mku wa majeshi ya ulinzi na kwa niaba ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Watanzania wote kwa ujumla, naomba nikukabidhi bendera ya Taifa, ambayo itakuwa ni kumbukumbu kuwa Hayati John Pombe Joseph Magufuli, kuwa amewahi kuongoza nchi hii kwa uadilifu na kwa kuwapenda Watanzania wote,” amesema mmoja wa maofisa wa JWTZ kabla ya kukabidhi bendera hiyo.

error: Content is protected !!