January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mallac ataka barabara zitunzwe

Daraja lililosombwa na mafuriko

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Annamery Stella Mallac (Chadema), ameitaka Serikali kutenga fedha za kutengeneza mitaro ili kuokoa kiasi kinachotumika kwa ajili ya kukarabati barabara zinazosombwa na maji. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kwa mujibu wa Mallac, serikali imekuwa ikitenga fedha nyingi kila mwaka kwa ajili ya matengenezo ya barabara za halmashauri za miji na wilaya ikiwemo za Mpanda na Sumbawanga zinazoharibika kutokana na ukosefu wa mitaro.

“Lini serikali itatenga fedha za kutengeneza mitaro hiyo ili kuokoa fedha zinazotumika mara kwa mara kutengeneza barabara zinazosombwa na maji? Amehoji. 

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim Majaliwa amesema serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa mitaro katika barabara za mijini.

Amefafanua kuwa, katika halmashauri ya Mpanda kuanzia mwaka wa fedha 2012/13 hadi 2014/15, jumla ya Sh. 502 milioni 502 zimetumika kujenga mitaro ya maji ya mvua.

“Kwa sasa Mji wa Mpanda una km 20.2 za mitaro ya maji ya mvua,”amesema Majaliwa na kuongeza kuwa, kwa kuzingatia mtandao wa barabara uliopo katika mji huo, jumla ya km 251.8 za mitaro ya maji ya mvua zinahitajika.

Aidha, amesema katika bajeti ya 2015/16, Sh. 150 milioni zimeombwa kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua katika barabara za Mji wa Mpanda.

error: Content is protected !!