Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Malkia Ladies kuwakutanisha wanawake 6,000 Dar
Michezo

Malkia Ladies kuwakutanisha wanawake 6,000 Dar

Spread the love

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, atakuwa mgeni rasmi wa kongamano la uwezeshaji wanawake kiuchumi, litakalo Jumamosi hii tarehe 20 Novemba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kongamano hilo litakalowakutanisha zaidi ya wanawake 6,000 litafanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba, jijini Dar es Salaam na kuratibiwa na kikundi cha Malkia Ladies na litahusisha washiriki wanawake likiwa na kaulimbiu ya ‘Mwanamke ni Nguzo ya Uchumi, Amka Uwekeze.’

Aidha, litatumika kuzindua kikundi hicho, Kampuni ya Bima, ramani ya jengo la biashara (Malkia Woman Market Mall) na Chaneli ya YouTube (Malkia Ladies Tv).

Malkia Ladies ni Kikundi cha Kikoba chenye wajumbe 34, kilichosajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwa lengo la kuwasaidia wanawake kupitia elimu ya fedha kwa maana ya uwekaji akiba na uwekezaji kwa maendeleo yao na familia zao.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Jumatano tarehe 17 Novemba 2021, Mwenyekiti wa Malkia Ladies Group, Charity Mwakalonge, alisema kongamano hilo linalenga kuwanoa wanawake juu ya namna bora ya kuanzisha na kuviendeleza vikundi kwa ustawi wa biashara na miradi wanayofanya na kuiendesha, ili vilete tija miongoni mwao.

“Sisi kwa mfano tuko wajumbe 34, ambako mzunguko wetu wa fedha kwa mwaka ni takribani Sh.250 milioni na hii imetokana na kikundi chetu kuwa na nidhamu ya uwekaji akiba na kuanza uwekezaji kupitia fursa mbalimbali na ndipo tukaja na wazo la Kongamano hili, ili kuwasaidia wanawake wengine,” alisema

“Tunawakaribisha wanawake wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla, kushiriki tamasha hilo litalofanyika kwa mfumo wa kongamano. Lengo ni kuwasaidia kujua namna sahihi ya kuanzisha na kuendeleza vikundi, pia tutachagua vikundi vitatu bora vitakavyoshiriki ambavyo kwa kuanzia tutavilea hadi vifikie kiwango kikubwa zaidi yetu,” alisema

Charity alisema, meni rasmi atakuwa Waziri Jenista Mhagama, atakayeambatana na Mlezi wa kikundi hicho, Getrude Mongella.

“Tuko tayari kuwapokea na kuwapa elimu wanawake wote watakaojitokeza na wito wangu kwao ni kuja kwa wingi na tunawakikishia hawatotoka bure, wataondoka na elimu kubwa itakayowasaidia kujenga na kubadili maisha yao,” alisema Mwakalonge.

Alifafanua kuwa pia watazindua Kampuni ya Bima itakayoanza kutoa huduma hivi karibuni, ramani ya jengo la maduka 100 ya wanawake kuuzia bidhaa zao, kitabu cha fursa 50, pamoja na Chaneli ya Malkia Ladies Tv ambayo itakuwa chachu ya akina mama kupata elimu ya masuala ya vikundi na uwekezaji, itakayotolewa kupitia mada na watoa mada tofauti, akiwamo Aunt Sadaka.

Kwa nyakati tofauti, Husna Mkupete ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Jamii na Chevawe Mberesero ambaye ni Mwenyekiti Kamati ya Uwekezaji, walitoa wito kwa wanawake mmoja mmoja ama vikundi kujitokeza kwa wingi PTA Jumamosi, ili kupigwa msasa utakaowawezesha kutekeleza majukumu yao kibiashara na kijasiriamali kwa weredi na kukuza pato lao na vikundi vyao.

Kongamano hilo linalotarajia kuwakutanisha pamoja zaidi ya wanawake 6,000 kuanzia asubuhi hadi jioni, litapambwa na burudani kamambe kutoka kwa msanii mkali wa dansi Aneth Kushaba na The Star Band, pamoja nyota wa Bongo Fleva, Peter Msechu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!