July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Malkia Elizabeth awapa tuzo Watanzania

Malkia Elizabeth wa Uingereza

Spread the love

MALKIA Elizabeth wa Uingereza jana jioni aliwatunuku vijana wawili wa Tanzania tuzo ya kutambua mchango wa kama vijana ijulikanayo kama “Queens Young Leder’s Awards.” Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Waliotunukiwa ni Angela  Benedicto na Given Edward kutokana na kutambua mchango wa kazi zao katika kusaidia jamii.

Watanzania hao ni miongoni mwa vijana 60 wenye umri kati ya miaka 18 – 29 kutoka nchi za Jumuiya ya Madola ambao wametunukiwa tuzo hiyo katika makazi ya Malkia ya Buckingham Palace jijini London.

Akizungumza na MwanaHALISI online leo akiwa jijini London Angela (27) ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendeji wa Shirika la “Wote Sawa” la jijini Mwanza, linalofanya utetezi kwa wafanyakazi wa majumbani amesema, “Nimeipokea tuzo hii kwa furaha kubwa,” na kuongeza;

“Imenipa changamoto kubwa,  kwani hii tuzo ni kwa niaba ya wafanyakazi wa shirika la wafanyakazi wa nyumbani la Wote Sawa na kwa vijana viongozi wanaofanya kazi zao kwenye jamii.”

Aidha, Angela amesema kuwa, ana wajibu wa kufanya kazi kwa bidii kwa kujitolea ili asadie jamii yake. Anawashauri vijana kwamba “huu ni wakati wetu tuamke tutafute fursa na tuzitumie.”

Edward yeye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa MyElimu unaowawezesha wanafunzi wa shule za sekondari Tanzania kufanya mijadala katika masuala ya masomo.

Mbali na kupata tuzo pia watapata mafunzo ya mtandao yanayotolewa na Chuo Kikuu cha Cambridge cha nchini humo.

error: Content is protected !!