January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Malisa aagwa, Magereza wamlilia

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe akiuaga mwili wa Kamishna mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Elias Malisa

Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, awaongoza watumishi na watendaji wa wizara hiyo, kuaga mwili wa aliyekuwa Kamishna mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Elias Malisa. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Tukio hilo limefanyika leo Jijini Dar es Salaam, katika viwanja vya Chuo cha Maafisa Ukonga, ambapo viongozi mbalimbali na wananchi walijitokeza kutoa heshima zao za mwisho.

Malisa alifariki Juni 2 mwaka huu, akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Lugalo. Mwili wake unatarajiwa kusafirishwa kuelekea Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi kesho.

Akisoma wasifu wa Malisa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP), Gideon Danford Nkana, amesema, marehemu alizaliwa mwaka 1944, mkoani Kilimanjaro na kuaza shule ya msingi mwaka 1951 hadi 1958.

Nkana amesema, Malisa alihitimu kidato cha nne  mwaka 1974,  na baadae akasoma sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alitunukiwa shahada ya kwanza mwaka 1977.

Malisa alijiunga na Jeshi la Magereza mwaka 1964, baada ya kuhitimu mafunzo ya awali ya uaskari Magereza chuoni Ukonga, ambapoa alipata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya uongozi mbalimbali.

Aidha, “kutokana na utendaji wake kuwa mzuri, aliwahi kutunukiwa vyeo mbalimbali vipatavyo 11, kikiwemo cha ukuu wa Magereza mwaka 1992 hadi 2002 alipostaafu,” amesema Nkana.

Hata hivyo, Malisa aliwahi kufanya kazi katika vituo mbalimbali vikiwemo, Gereza la Butimba-Mwanza, Isanga- Dodoma, Wami vijana- Morogoro, Chuo cha Usalama –Moshi, Songwe-Mbeya, Chuo Ukonga- Dar, na Mkao makuu ya Jeshi la Magereza- Dar.

Pia, aliwahi kushika nyadhifa zipatazo 11, ikiwemo ya kuazisha sheria ya huduma kwa jamii. Mbali na hizo, amewahi kutunukiwa nishani 3 pindi akiwa kazini. Ameacha mjane na watoto watano.

Akimzungumzia Malisa, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu, amesema, “kwa hakika tumepoteza mtu muhimu sana katika idara yetu, kwani alikuwa ni kiongozi wa kuigwa na jamii.”

Mangu ameongeza, “hata baada ya kustaafu, Malisa aliendelea kuwa nasi na tumeshirikiana kwa vitu vingi ikiwemo na kutoa ushauri pale tunapopungukiwa, hakika nitamkumbuka sana kwa kazi zake.”

error: Content is protected !!